Jumatatu, 23 Mei 2016
SEmantik na pragmatiki . chuo kikuuu cha Arusha
CHUO KIKUU CHA ARUSHA
SHULE YA ELIMU
IDARA YA LUGHA NA FASIHI NA SANAA
JINA LA KOZI: KISWAHILI SEMANTICS AND PRAGMATICS
MSIMBO WA KOZI: KISE331
INAWASILISHWA KWA: FADHILI E.
INAWASILISHWA NA: MASOUD O. ISSA
NAMBA YA UTAMBULISHO: 201320484
Swali: 1. Jadili aina za maana ukitoa mifano kuntu toka mazingira halisi ya kiuanafunzi.
2. Nadharia za semantiki ni zipi? Na zinahalisikaje katika taalimu ya lugha isiyo rasmi?
Tarehe ya uwasilishaji ni Jumatano 20/04/2016,6:45.
DONDOO
UTANGULIZI.
Maana ya semantiki kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.
Maana ya pragmatiki kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.
KIINI.
Uhakiki kwa kutumia mifano mbalimbali katika lugha ya Kiswahili juu ya ukweli wa dai kuwa,pragmatiki huanzia pale ambapo semantiki huishia.
HITIMISHO.
Maoni ya wanakikundi.
MAREJEO.
Katika kujibu swali hili tutaanza na kufafanua dhana za msingi zilizo jitokeza katika swali letu kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali dhana hizo ni pamoja na; semantiki na pragmantiki. Baada ya kuzifasili maana hizo tutajikita kwenye kiini cha swali kuwa pragmantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia kisha tutahitimisha mjadala huu na mwisho tutaorodhesha marejeo.
Kwa kuanza na kufafanua maana ya semantiki ; wataalamu mbalimbali wanaeleza maana ya semantiki kwa namna tofautitofauti kama ifuatavyo;
Alfred (1933), anaeleza kuwa semantiki ni Nyanja inayojishughulisha na uchambuzi wa maana.
Naye Yule (1996),anamuunga mkono Alfred kwa kufafanua maana ya semantiki kuwa inajihusisha na uchambuzi wa maana katika neno na katika sentensi.
Pia Stuwart na Nathan (2001), na Habwe na Karanja (2004),wanafanana katika kuwafasili maana ya semantiki isipokuwa wanatofautiana katika istilahi kwani Stuwart na Nathan wanatumia dhana ya tawi la isimu wakati Habwe na Karanja wanatumia istilahi ya utanzu wa isimu. Lakini wote wanafafanua kuwa semantiki inajihusisha na uchambuzi wa maana katika lugha.
Hivyo basi kwa ujumla tunaweza kusema kwamba semantiki ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi wa maana katika lugha za binadadamu.
Pamoja na wataalamu hawa kujishughulisha na maana ya semantiki, hawakuishia hapo tu kwani walijishughulisha pia na maana ya pragmantiki kama inavyoelezwa hapa chini.
Bakari (1988) anaelaza kuwa pragmantiki ni maana ambapo mwandishi au msemaji amekusudia kuiwasilisha. Maana hii inatokana na muktadha wa mwadishi au msemaji.
Maana hii kwa kiasi Fulani imeonekana kuwa na udhaifu Fulani kwani anajikita zaidi katika muktadha wa msemaji au mwandishi kumbe basi pragmatiki ni sharti izingatie pia muktadha wa hadhira yaani msomaji na msikilizaji na sio muktadha wa msemaji au mwandishi tu.
Stuwart na Nathan (2001) wao wameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa pragmantiki inajihusisha na namna watu wanavyotumia lugha katika muktadha na kwa nini wanatumia lugha kwa namna hiyo.
Hivyo tunaweza kusema kuwa pragmantiki ni stadi inayochunguza maana kulingana na muktadha Fulani.
Baada ya kufafanua maana ya semantiki na pragmatiki , ufuatao ni uhakiki wa dai kuwa pragmantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia. Ni dhahiri kuwa pragimantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia kutokana na nyanja za maana kama vile maana ya msingi na maana ya ziada. Kwa sababu pragmantiki imekuwa kama suluhisho la mapungufu ya semantiki yaani pale ambapo semantiki imeshindwa kuelezea pragmantiki huendeleza; hii ni kutokana na ukweli kwamba semantiki huelezea maana ya msingi tu ya neno au sentensi wakati pragmantiki huelezea maana ya ziada. Ufuatao ni uthibitisho wa dai kuwa pragmantiki huishia pale ambapo semantiki huishia,kwa kuangalia mambo yafuatayo:
Maana na matumizi ya maneno; semantiki hueleza maana ya msingi lakini neno hilohilo linaloelezwa kisemantiki linapokuwa katika matumizi ndipo tunapata maana ya ziada ambayo ndio pragmantiki.
Mfano;
Neno simba ni mnyama mkali mwenye rangi ya majani makavu anayeishi porini.
Neno hilohilo simba linapokuwa katika matumizi linatupatia maana tofauti na ile ya msingi ambayo ndiyo maana ya kipragmantiki.
Mfano; Hakika kijana Yule ni simba kwelikweli; kinachomaanishwa hapa sio kijana Yule ni mnyama kama semantiki inavyoeleza bali kinachomaanishwa ni kuwa kijana Yule ana tabia kama za simba kwa maana kuwa ni mkali , hodari na ana nguvu sana. Hivyo tunaona kuwa pragmantiki inaenda mbali zaidi kutoka pale ambapo semantiki inaishia.
Matumizi ya methali mbalimbali, Methali ni semi fupifupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yanayotokana na uzoefu wa kijamii. Katika kuangalia methali tunaangalia maana ya kisemantiki na ya kipragmatiki mfano methali kama
“mgaagaa na upwa hali wali mkavu”. katika methali hii maana ya msingi (maana ya kisemantiki) ni kuwa mtu anayezunguka katika ufukwe wa bahari hawezi kula wali mkavu. Hapa tunaona pragmantiki inaenda mbali zaidi kwa kuifafanua methali hii kuwa mtu yeyote anayejishughulisha hawezi kukosa riziki. Hivyo dai la kuwa pragmantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia ndipo linapojidhihirisha.
“Aisifiaye mvua imemnyea” maana ya msingi au ya kisemantiki tunayoipata hapa ni kwamba anayeisifia mvua huwa imemnyeshea. Lakini pragimantiki inaendelea mbele zaidi kwa kuifafanua methali hiihii kuwa wepesi au uzito wa jambo anaujua yule liliyemkuta; ni vigumu sana kwa mtu ambaye hajafikwa na tatizo kuweza kuelewa uzito hasa wa tatizo hilo.
“Mkono mmoja hauchinji ng’ombe” katika methali hii maana ya kisemantiki ni kuwa mkono mmoja hauwezi kuchinja ng’ombe; lakini pragmantiki inaendelea mbali zaidi kwamba ili jambo lifanikiwe/ kufanikiwa kwa jambo kunahitaji ushirikiano.
“Mgema akisifiwa tembo hulitia maji” maana ya kisemantiki katika methali hii ni kuwa mtengenezaji wa pombe akisifiwa tembo (mnyama) hutia maji; hapa tunaona pragmantiki inaanzia hapo na kwenda mbali zaidi kufafanua methali hii kuwa mfanya jambo likaenda na sifa mweshowe hufanya tadi au jeuri.
Hivyo kutokana na methali hizo hapo juu msikilizaji kama atazingatia maana ya kisemantiki tu (maana msingi) hawezi kupata ujumbe uliolengwa na msemaji au mwandishi ipasavyo, hivyo ili kuupata ujumbe uliokusudiwa na mwandishi au msemaji atahitaji azingatie maana ya kipragmantiki na kwa kuzingatia maana ya kipragmantiki basi atauelewa ujumbe wa methali hizo vizuri hivyo kutokana na hilo tunathibitisha kuwa pragmantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia.
Matumizi ya semi mbalimbali; semi ni fungu la maneno linalotumiwa na jamii ya watu kwa namna maalumu ili kutoa maadili. Mfano wa semi;
“Biashara haigombwi” katika usemi huu maana ya msingi (kisemantiki) ni kuwa biashara haigombaniwi; lakini pragmantiki inaendeleza kutoka katika maana hii ya kisemantiki kwa kueleza maana ya methali hii kuwa ni busara mchuuzi kuwabembeleza wanunuzi wake.
“Cha mlevi huliwa na mgema” katika usemi huu maana ya kisemantiki ni kuwa kitu cha mlevi huliwa na mtengenezaji wa pombe, lakini pragmantiki inakwenda mbali zaidi ya semantiki kwani inafafanua maana ya usemi huu kuwa mali ya mtu asiyeithamini huwanufaisha watu wengine.
Matumizi ya nahau mbalimbali, ni fungu la maneno lenye maana maalumu isiyotokana na maana ya kawaida za maneno hayo; katika nahau semantiki hutoa maana kulingana na maneno yaliyojitokeza katika nahau hiyo, hivyo huwa si rahisi kupata maana haswa iliyokusudiwa na msanii kwani ili kuipata maana hiyo ni shariti kurejelea maana ya kimuktadha (maana ya kipragmantiki) mfano wa nahau ni;
“Chinjia baharini” katika nahau hii maana ya msingi ni kuwa chinjia eneo lenye maji ya chumvi, hivyo kutokana na maana hii ya kisemantiki msikilizaji hawezi kupata maana ile iliyokusudiwa hivyo kutokana na hilo pengo pragmantiki inakamilisha kwa kuufafanua msemo huo kwamba ni nyang’anya au dhulumu.
“zunguka mbuyu ” maana ya ya kisemantiki katika nahau hii ni kitendo cha kugeuka kwenda upande mmoja wa mti mkubwa mnene sana wenye shina lenye nyuzinyuzi tu bila ya kubadili nafasi. Hivyo kutokana na maana hiyo ya msingi msikilizaji hawezi kupata maana hasa iliyokusudiwa na msemaji kwa maana hiyo tunaona kuwa pragmantiki inaenda mbali zaidi kuwa kuzunguka mbuyu ni kula rushwa.
Pia ukweli wa dai hili kuwa pragmantiki huanzia pale semantiki inapoishia unaweza kudhihirishwa kwa kutumia mahusiano ya kifahiwa ambayo ni mahusiano ya maana ya maneno yanayounda kikoa kimoja cha maana kama ifuatavyo.
Katika leksimu moja kuwa na maana nyingi zisizohusiana; mfano paa,kaa,pamba na panda ambapo kisemantiki maneno haya huwa na maana nyingi zisizohusiana na hivyo huleta utegemezi wa kimuktadha ili kupata maana kuntu na hapo ndipo pragmantiki inapofanya kazi iliyoachwa na semsntiki.
Vilevile katika semantiki kuna maneno ambayo huwa na maana nyingi zinazohusiana mfano “nguzo” na “mama” na hivyo uelewekaji wake hutegemea muktadha husika. Mfano neno “mama” maana yake ni asili, mzazi wa kike hivyo basi utumikaji wa neno hili katika sentensi huweza kuwa na maana tofautitofauti kulingana na muktadha. Mfano chuo cha Dar es salaam ni chuo mama hapa Tanzania.
Pia katika hali ya sentensi kuwa na maana zaidi ya moja au kueleweka kwa namna tofautitofauti ndipo pragmantiki hufanya kazi katika kueleza maana ya kimuktadha au maana ya ziada. Mfano,Juma anapanda hii inamaana ya kuwa;
Anasia mbegu
Anakwea mlima au mti
Sehemu ya tawi la mti
Hinyo basi katika kupata maana halisi ya manenoya namna hii hatuna budi kuhusisha na muktadha husika.
Ukweli mwingine wa dai hili tunaupata katika maneno ya ukinzani au vigambe viwili siganifu vinavyofanya kazi wakati mmoja; mfano, mtoto Yule ni mtu mzima kwelikweli.(+ mtoto,-mtoto) hapa maana ya kisemantiki ni kuwa mtoto huyu ni mtu mzima lakini pragmantiki inaenda mbali zaidi kwa kufafanua kuwa mtoto huyu anatabia za watu wazima mfano matendo yake; mfano mwingine ni kucheka huko ndiko kulia kwenyeweHivyo ubainishaji maana katika kauli hizi hutegemea muktadha ambapo neno hilo limetumika.
Vilevile dai hili huweza kuthibitishwa katika vimanilizi ambapo mtu hugundua maana ya jambo Fulani kupitia yanayosemwa na msemaji. Mfano( mazungumzo kati ya A na B)
a/ leo utaenda chuo
b/ sina kipindi
hivyo kutokana na mazungumzo hayo tunapata kimanilizi kuwa a/ hataenda chuo maana ambayo ni ya kipragmatiki na ambayo haielezwi na semantiki.
a/ vipi utaoga leo?
b/ kuna baridi.
Kutokana na mazungumzo hayo kimanilizi tunachokipata ni kuwa b/ hataoga maana isiyoelezwa na semantiki bali huelezwa na pragmantiki.
Kwa kuhitimisha ikumbukwe kwamba licha ya dai kuwa pragmantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia hua na mashiko kwa kiasi Fulani lakini dhana zote mbili hutegemeana kwa kiasi kikubwa kwani maana ya ziada ambayo ndiyo ya kipragmatiki hujengwa au hutokana na maana ya msingi yaani maana inayochunguzwa na semantiki.
MAREJEO
Bakari, N (1988),Analysis of Modern Swahili Texts and Language Skills. University of Nairobi.
Habwe, J na P. Karanja (2004), Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi. Phoenix publishes.
Stuwart, T na V. Nathan (2001), Language files ( 8th Ed).The Ohio State University.
Yule, G (1996), Pragmatic.London and New York.OUP
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
TAASISI YA TAALUMA ZA KISWAHILI
IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU
KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMANTIKI YA KISWAHILI
MAHALI: ARD
MUDA: 08:00- 09:00 MCHANA
SIKU YA SEMINA: ALHAMISI
WANAFUNZI WALIOSHIRIKI
NAMBA JINA NA. USAJILI KOZI SAHIHI
1 SANGA HADIJA, A 2010-04-07156 BAK
2 BUSHIRI ZAKIA 2010-04-03405 BAK
3 TEMBA AGNESS.V 2010-04-05700 BAK
4 JOHANSEN HAPPINESS 2010-04-03283 BAK
5 ULOMI JOYCE 2010-04-03973 BAED
6 MINIPH JUDITH 2010-04-04365 BAED
7 MABULA KUND,S 2010-04-01046 BAED
8 MKONO ELIZABETH 2010-04-01678 BAED
9 BELEKO MARIAM 2010-04-01499 BAK
10 HAMAD AZIZA 2010-04-02778 BAK
11 MSIMUHE TUMAINI 2010-04-01223 DAED
12 NAMBENE HILDA 2010-04-00112 BAED
13 KANISA GRACE 2010-04-05041 BAED
14 ABDALAH MARIAM 2010-04-03359 BAED
15 BUSAGALA ZEPHANIA 2010-04-07149 BAED
16 MASINGA JAMES, M 2010-04-05502 BAED
17 BHOKE NYAIBULI 2010-04-03166 BAED
18 LAURENT ANNA 2010-04-04857 BAED
SWALI.
Pragmantiki huanzia pale ambapo semantiki huishia. Hakiki ukweli wa dai hili kwa kutoa mifano murua na yakutosha kutoka katika lugha ya Kiswahili.
Maarifa ya lugha ni elimu ya kupambanua vijengo mbalimbali vya lugha na kanuni zake kulingana na taratibu za lugha hio. Ulimwengu halisi ni mukatadha ambao maarifa ya lugha huweza kutumika ili kuleta taathira kama ilivyokusudiwa na msemaji au mwandishi. Richmond Thomason (2012) anafafanua maana ya semantiki kwamba ni tawi la isimu ya lugha linalohusu maana za viyambo vya lugha. Hivyo basi ni kusema kuwa, semantiki ni utanzu wa isimu unaojishughulisha na maana ya maneno au viyambo vya maneno katika lugha. Swali kuu katika wanasemantiki ni kuhusu ninini maana ya maana. Hata hivyo wanasemantiki hujikita katika kuchunguza maana katika viwango mbalimbali kama vile; ngazi ya sauti (fonimu), neno, virai, vishazi na hata sentensi. Tawi hili la isimu limekuwa ni muhimu sana hasa kutokana na umuhimu wa mazungumzo, kwani ili mazungumzo yaeleweke na ujumbe ufahamike panahitajika maana. Aidha nivyema ifahamike kuwa semantiki inajihusisha na maana za maneno kiisimu, kwani maana yake hupatikana kutokana na muundo wa maneno hayo au maarifa ya lugha husika. Kwa upande wa pragmatiki Richmond Thomason (2012), anasema kwamba ni tawi la lugha linalojihusisha na matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha wa wazungumzaji walugha husika. Hivyo Thomson anadai kuwa pragmatiki inahusu zaidi mambo mawili; matumizi na muktadha. Geoffrey Finch (2000) anasema kuwa, dhana ya pragmatiki ilivumbuliwa katika miaka ya 1930 na mwanafalsafa C.W. Morris, na imeanza kujulikana kama tawi tegemezi la isimu lugha miaka ya 1970 ambapo kabla ya hapo pragmatiki ilihusishwa kama tawi la kifalsafa, na kufafanuliwa kwa kuzingatia misingi mikuu miwili; matumizi na muktadha. Kuanazia miaka ya 80 wataaklamu walianza kuiangalia pragmatiki kama maana ya msemaji na tafsiri kilichosemwa, yaani maana ya msikilizaji. Kwa upande wake Yule (1996) anafafanua dhana ya pragmatiki kwa kusema kuwa ni taaluma inayohusu mahusiano yaliyopo kati ya maana ya lugha na watumiaji wa mambo hayo. Betty J. Birner (2012) anasema kuwa dhana hizi ni dhana zinazoshabihiana. Tofauti kubwa iliyopo kati ya dhana hizi bado ni mjadala mpana kwa baadhi ya wanaisimu wa lugha, hii ni kwa sababu, pragmatiki na semantiki zinajishughulisha na maana, kwa hio zipo hisia za ukaribu mno katika taaluma hizi mbili, licha kwamba pia zipo hisia za karibu za kuonesha utofauti wao. Niukweli usiopingika kwamba kuna maarifa ya lugha na wakati huohuo kuna maarifa ya ulimwengu halisi, hii inamaana kuwa kufahamu lugha peke yake haitoshi lazima lugha hiyo itumike kulingana na muktadha au ulimwengu halisi ambapo lugha hio imetumika. Hali hii inaweza kuthibitishwa kutokana na kuwepo kwa matumizi ya maana tofauti kwa kadri ya watumiaji husika kama ifuatavyo. Matumizi ya maana ya msingi katika kufafanua maana. Hii ndiyo njia kuu ya kulipa neno maana, ambayo kwa kawaida haibadiliki kutegemeana na athari za kimazingira. Hii inamaana kuwa maana ya neno au tungo itabaki ile ile hata kama mazingira yatabadilika. Maaaana hii ndiyo inayojulikana kama maana ya kileksika. Kwa mfano; kichwa- kikimaanisha sehemu muhimu katika mwili wa binaadamu kinachokusanya viungo kama vile; macho, masikio, pua na mdomo. Hii ndiyo maana pekeyake inayohitaji ulimwengu wa lugha kwa kiwango kidogo sana, hata hivyo bado ulimwengu halisi utahitajika kutokana na matumizi ya maneno kama vile homophoni na homonimia. Mfano neno kama kaa licha ya kuwepo kwa maarifa ya lugha lakini bado maarifa yaulimwengu halisi yanahitajika kuelewa kusudio la mzungumzaji, kwani yapo mazingira ambayo neno hilo litaendelea kutumika kama kitendo cha kuketi, na mazingira mengine litumike kama cheche la moto, na yote hayo ni maana ya msingi ya neno kulingana na miktadha tofauti tofauti. Maana ya ziada au kisarufi. Ni maana abayo huibuka kutokana na maana ya msingi. Maana hii inatudhihirishia kuwepo kwa maarifa ya lugha na wakati huohuo kuna maarifa ya ulimwengu halisi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, maana hizi hutegemeana na kuhusiana na mazingira halisi ya matumizi. Kuelewa maana ya ziada sio tu kuelewa maarifa ya lugha, bali pia ulimwengu halisi au muktadha ambapo maneno au fahiwa hizo zimetumika. Mfano pale mzungumzajia atakapo sema “Samahani kaka! Hivi utaendelea kuwa kupe hadi lini? haya ni maisha tu!” utagundua kuwa, hapa kufahamu maana ya tungo hii si kutokana tu na kufahamu maarifa ya lugha, lakini pia inahitajika ufahamu wa ulimwengu halisi ambao tungo hio imetumika, kwa kusema kupe kumaaanisha mtu mnyonyaji au mtegemezi. Maana ya kimtindo. Hii ni maana inayohusiana moja kwa moja na matumizi ya lugha kulingana na muktadha husika. Katika aina hii ya maana, neno au kiyambo hupata maana kulingana na mtindo ambao neno au kiyambo hicho kimetumika. Mfano mtindo wa kilahaja, mtindo wa wakati, mtindo wa kieneo, au hata mtindo wa taaluma ua fani fulani. Ni lazima tukiri kwamba kuna marifa ya lugha lakini wakati huo huo kuna ulimwengu halisi. Hii ni kwa maana kwamba katika maana hii, lazima mtumiaji wa lugha licha ya kufahamu maarifa ya lugha hio, lakini lazima azingatie ulimwengu halisi ambao lugha hio imetumika. Mfano matumizi ya mtindo wa kilahaja, kuna baadhi ya maneno kiuhalisia huibua hisia zingine na wakati mwingine kushindwa kufahamika kutokana na tofauti za kilahaja. Mfano maneno kama vile, shule, ugali na bomba, maneno haya yanaweza kutumika katika hali tofauti kwa wakaazi wa Tanzania bara na visiwa vya Zanzibar. Kwa upande wa Zanzibar wangeweza kutumia skuli, sembe na mfereji kwa mfuatano. Hivyo basi, kwa mzungumzaji inampasa kujua ni akina nani anazungumza nao na nani wangeweza kumuelewa ingawa wate wana maarifa ya lugha moja. Aidha, kuwepo kwa maana hisia ni ithibati tosha ya kuthibitisha kuwepo kwa maarifa ya lugha na wakati huohuo ulimwengu halisi katika dhana ya semantiki na pragmatiki zinazohusu maana. Tunapozungumzia maana ya hisia ni aina ya maana ambayo huibuka kutokana na hisia au mtazamo wa msemaji au mwandishi. Na maana hii huweza kuwasilishwa kwa njia mbalimabali zikiwemo, njia ya maana kama dokezi au njia isiyo ya moja kwa moja. Kwa mfano “kweli wewe ni kidume wa mbegu kwelikweli!” katika tungo hii ni vigumu kufahamu mzungumzaji amemaanisha nini ikiwa msikilizaji hatohusisha maana au kauli hii na ulimwengu halisi au muktadha ambao msemaji au mwandishi amezungumza au kukusudia, kwani maana ya msemaji itakua tofauti na maana ya msikilizaji atakayojengwa kwa kuzingatia tu maarifa ya lugha. Mathalani hapa tunaweza kusema kuwa, msemaji amekusudia huyu kijana ni mchapakazi kwelikweli. Au kwa waswahili wanakawaida ya kumsifia mtu kwa kusema kwa mfamo, huyu mchezaji yaani hafai, mshenzi kwelikweli! Kiuhalisia neno hafai linamaanisha hali hasi ya mtu, vile vile mshenzi ni neno linalotaswira mbaya ya ufedheheshaji, lakini waswahili husema hivyo kuonesha sifa njema za mtu, tofauti n auhalisia. Hivyo kwa mtu kufasiri maana kulingana na maarifa ya lugha inapelekea kupotosha maana iliyokusudiwa. Maana tangamani. Hii ni maana inayopatikana kutokana na matumizi ya lugha kulingana na muktadha husika wa matumizi kwa kuzingatia maana ya maneno mbalimbali na jinsi yanavyotumiwa kwa pamoja ili kuleta maana iliyokusudiwa. Maana hii pia inatuthibitishia kuwepo kwa maariufa ya lugha na wakati huohuo ulimwengu halisi. Hii inamana kuwa si kujua tu maariufa ya lugha ndio kuweza kuitumia lugha hio, lakini ni kwa vipi lugha hio ingeweza kutumika. Kwa mfano kauli kama vile “Mabibi na mabwana”, mvulan amtanashati, dada mrembo. Ukichunguza tungo hizi utagundua kuwa si kufahamu tu maarifa ya lugha, bali lazima mtumiaji afahamu ulimwengu halkisi wa matumizi ya maneno hayo. Mfano msemaji angeweza kusema, ‘mabibi na mababu” au “dada mtanashati” na ‘mvulana mrembo” jambo ambalo lisengekubalika kajika jamii za waswahili. Maana mangwi au akise. Ni aina ya maana ambayo huibuka katika hali ambayo maana moja hukonyeza maana nyingine na hivyo humfanya mtu afikirie maana nyingine pia. Mfano kauli “naenda kujisaidia” Katik tungo hii inahitaji mtumiaji wa lugha au msikilizaji kufahamu ulimwengu halisi, yaani wanajamii fulani wanavyosema kujisaidia wanamaanisha nini? Kwa mfano mara nyingio katika jamii za kiafrika kujisaidia humaanisha ima kuenda haja ndogo au kubwa. Jambo hili katu lisengefahamika kwa sababu tu ya kufahamu maariga ya lugha hio. Mwisho ni maana ya dhamira au muhimu. Hii ni aina ya maana ambayo hutegemea kile ambacho mtoa ujumbe ana kipa umuhimu zaidi. Mara nyingi kile kinachopewa umuhimu zaidi hutokeza mwanzoni mwa senmtensi. Msingi wa kupata maana katika aina hii inathibitisha kuwa pamoja na kuwa na marifa ya lugha pia panakuwepo n aulimwengui halisi wa lugha. Kupitia aina hii ni vigumu mtu kutambua umuhimu wa msemaji au mzungumzaji kwa msingi tu wa maarifa ya lugha bila kuhusisha hali gani lugha hio imetimika. Mfano kauli ya kusema “Kikwete atashinda uchaguzi wa mwaka 2015” Katika mfano huu umuhimu zaidi upo kwa Kikwete ndiye ambaye ana tarajiwa kushindsa uchaguzi na sio uchaguzi wala mwaka 2015. Haya yote yatabainika ikiwa tu msikilizaji atakuwa anamaarifa ya lugha na wakati huohuo anaujua ulimwegu halisi. Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, semantiki na pragmatiki zote kwa pamoja zinahusiana, kwa mana kwamba zinajihusisha na maana ya maana katika lugha. Wala haitokuwa sahihi kudhani kwamba kufahamu tu maana ya viambajengo katika tungo, iwe neno, kirai, kishazi au hata sentensi kuwa ndio kufahamu kwa kile kilichokusudiwa bila kujali muktadha ambao neno hilo imetumika. Hat hivyo, taaluma hizi bado zitaendelea kuwa tofauti kwa kuwa semantiki hujihusisha na maana za maneno au viyambo vya maneno kama vilivyo kupitia kwa masemaji na msikilizaji. Wakati huohuo pragmatiki hujishughulisha na jinsi gani muktadha unapelekea kupata maana ya kile kilichokusudiwa kulingana na muda mahsusi. Aidha ifahamike kuwa Semantiki na Pragmatiki zote kwa pamoja zimelenga kutoa ufafanuzi kuhusu mchakato wa lugha na matumizi yake kulingana na muktadha wa uzungumzaji au utumikaji wake. Kama sehemu ya mfumo wa mazungumzo , sambamba na kufasiri na kufafanua mfumo fungamanifu wa mazungumzo katika lugha, na hili litafikiwa tu kwa kuzingatia maarifa ya lugha sambamba na ulimwengu halisi wa mazungumzo. MAREJEO. Geoffrey Finch, (2000). Linguistic Terms and Concepts. Palgrave Macmillan. Jacob L. Mey, (2001). Pragmatics: An Introduction, 2nd ed. Wiley-Blackwell. Richmond H Thomason (2012). What is semantics? Second version. Wwww.wisegeek.com Publishing & Printing International Journal. (USA), downloaded on Friday, 30th May 2014, at 12:30 pm. Yule, G. (1996). Pragmatics. Oxford: Oxford University Press.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ
Semantiki
Semantiki (Hasa huitwa: Sarufi maana) ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa maana za maneno au tungo katika lugha. Ni taaluma inayochunguza na kuchambua maana ya hisia na vitu halisi kimaneno na matumizi ya maneno kwa ujumla kisayansi. Weledi wa semantiki kwa mtumiaji ndio humsaidia mtumizi wa lugha kuitumia kwa ufaafu na kwa maadili ya mazingira husika.
Sayansi inayozungumzwa hapa ni ile ambapo lugha huchunguzwa na kuchambuliwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu maalumu zinazoihusu lugha husika. Hivyo basi kitendo cha kufuata kanuni na taratibu katika uchunguzi na uchambuzi wa lugha ni kigezo cha kisayansi.
Matawi ya isimu ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Kwa mtazamo huo wa jumla wa isimu, maana ya semantiki yaweza kujengwa katika muonekano ufuatao. Semantiki ni tawi la isimu au taaluma ya isimu ambayo hufuata kanuni na taratibu maalumu katika kuchunguza na kuchambua maana katika lugha. Maana hizo zaweza kuwa katika maneno, vifungu au sentensi, pia maana zinazoshugulikiwa ni zote, ziwe za wazi au zilizojificha.
Mifano
Maana iliyowazi (maana nyoofu/nyofu)
Maana isiyowazi (maana tata)
Jinsi ya kuondoa utata katika tungo hizo katika SENTENSI NA TUNGO KWA UJUMLA
Mifano ya maana tata
Paka (paka mnyama au paka rangi ya kitu fulani - pia kwa maneno ya msimu paka = kumwambia mtu ukweli kwa kutumia sauti ya juu bila kujali kama atakereka au la).
Panda (panda ngazi au mlima. Vilevile ni hali ya kupanda mbegu za kitu fulani ardhini ili upate mazao kama vile maharagwe, mahindi, mchele, n.k).
Kaa (kaa chini au katika kiti - vilevile kaa samaki).
1
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
1
SEMANTIKI/MAANA YA MSINGI
Kwa mujibu wa Crystal (1987) semantiki ni utanzu wa isimu unaochunguza maana katika lugha.
Hii inamaanisha kwamba semantiki hutalii maana katika vipashio vyote vya kiisimu katika
viwango vyote vya lugha yaani fonolojia, mofolojia na sintakisia. Au semantiki inaweza kufasiliwa
kwa namna mbalimbali kama vile;-
• Semantiki ni stadi ya maana
• Semantiki ni utanzu wa isimu unaongalia maana ya maana
• Semantiki huchunguza lugha za binadamu kwa viwango vya sauti, maneno, virai na hata
sentensi.
Katika semantiki kitu cha muhimu sana ambacho kinaangaliwa ni maana katika lugha za
binadamu.
Sababu ya kuchunguza maana katika lugha za binadamu ni kuwa:-
• Kazi kuu ya lugha ni mawasiliano ambayo huhusisha upatikanaji wa habari, taarifa au
ujumbe
• Ili ujumbe huo ueleweke ni lazima pawe na maana ya kisemwacho kwa msikilizaji. Kwa
hiyo kama ambavyo tumedokeza hapo juu kwamba katika kutafuta maana lazima
viwango vyote vya isimu vihusishwe (Fonolojia, Mofolojia na Sintakisia).
• Semantiki ndiyo inayounganisha nyanja hizi zote. Kwa namna moja au nyingine tunaweza
kusema kwamba pasipokuwa na semantiki matawi mengine hayawezi kufanya kazi kwa
sababu matawi haya yote yanahitaji kuchanuza maana ambapo semantiki inajishughulisha
nayo. Kwa hiyo kuna uhusiano wa moja kwa moja kwenye semantiki. Tazama mchoro wa
mahusiano hayo. Hapa semantiki ipo katikati kwa sababu inahusika katika nyanja zote
Kwa hiyo semantiki ndiyo inayounganisha matawi haya yote
MAMBO YANAYOSHUGHULIKIWA NA SEMANTIKI
a) Maana ya maana na uainishaji wa maana za maneno
b) Maana za tungo
c) Etimolojia ya maana za maneno
d) Uhusiano wa kimaana katika maneno
e) Uhusiano wa kimaana katika tungo
f) Nadharia za uchambuzi wa maana
FONOLOJI MOFOLOJI
SEMANTIKI
SINTAKSIA
2
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
2
Ufafanuzi wa mambo haya ni kama ifuatavyo:-
A. MAANA YA MAANA
Maana ya maana huchunguzwa katika viwango vikuu viwili:-
a) Katika neno huru (leksia)
b) Katika kiwango cha tungo (kisarufi)
Ili kumudu taaluma ya semantiki (yaani ili uweze kuchambua maana kwa ngazi ya lekisia
na kisarufi) ujuzi wa muundo wa lugha na utamaduni wake vinahitajika sana. Hii ni sawa
na kusema kuwa huwezi kuchambua maana katika lugha ambayo huelewi miundo yake na
utamaduni wake.
Hata hivyo, Maana ya maana bado ni ngumu na ina utata sana. Matinde (2012:237)
anasema neno maana hudokeza fahiwa (sense) nyingi sana. Mifano ifuatayo inaonyesha
utata wa neno maana katika kila sentensi linamotumika
i. Una maana gani kutojibu sms yangu?
ii. Kufuka kwa moshi kuna maana kuwa mahali hapo kuna moto
iii. Mchoro wa fuvu la binadamu una maana ya hatari
iv. Neno mrupo lina maana gani?
v. Mradi huu una maana kubwa sana kwetu
vi. Asiyejua maana haambiwi maana
vii. Kumbe yule jamaa hana maana hata kidogo
viii. Kweli nilisema hivyo lakini sikumaanisha
ix. Juzi ilinyesha mvua ya maana maeneo ya Moshi
x. Ulimwita mwenzio mama ukiwa na maana gani wakati ukijua yeye ni
mwanamume
xi. Naenda kuandika notisi maana kozi yenyewe imepinda
Kutokana na fasili hizi za maana tunaweza kugundua kuwa kuna utata mkubwa juu ya
neno ‗maana‘ kwani linadokeza fahiwa zisizo na ukomo. Hata hivyo uchunguzi wa sifa za
ufasiri wa maana ni sehemu muhimu katika taaluma ya semantiki au isimu maana.
ALAMA/ISHARA NA MAANA
Taaluma ya semantiki ni taaluma ndogo katika taaluma iitwayo Semiotiki au Semiolojia.
Semiolojia/ semiotiki ni taaluma ya alama na ishara katika kuashiria maana Wakati
semantiki huchunguza alama za lugha za binadamu na maana zake, semiolojia huangalia
alama na ishara mbalimbali katika kupata maana mbalimbali.
Kuna aina tatu za ishara
i. Ishara za usababisho/index
kuna kufungamana kwa kiusababishano kati ya alama au ishara na kile kinachoashiriwa.
Yaani jambo moja husababisha jambo la pili. Kwa mfano:
Moshi-alama ya moto
Mawingu-alama ya mvua
ii. Ishara za ufananisho/ icons
Hapa kufanana kwa kipicha kati ya ishara na kinachoashiriwa. Kwa mfano picha ya mtu
ke/me katika milango ya vyoo. Au mchoro wa kitu na kitu chenyewe. Mfano ramani ya
nyumba, picha ya mtu.
iii. Ishara za nasibu au ishara nasibu
3
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
3
Katika ishara hizi hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ishara na kitu
kinachoashiriwa lakini uelewekaji wake hutokana na mazoea tu. Kwa mfano jina la mtu.
Ishara hizi ndizo zilizopo katika lugha kwa kiasi kikubwa ingawa ishara za usababisho na
ufananisho zipo pia. Kwa mfano Bendera kama kiashiria cha kikundi/chama/nchi
inayoiwakilisha. Rangi nyekundu kama kiashiria cha hatari/mapenzi nk
NYANJA KUU ZA KUANGALIA MAANA YA MAANA
Maana ya maana huangaliwa katika Nyanja kuu mbili:- Maana ya msingi na Maana ya
ziada. Hebu tufafanue zaidi dhana hizi mbili.
i) Maana ya Msingi (Maana ya Kileksia)
Hii ndiyo maana kuu ya neno, maana hii haibadiliki kwa kutegemea mabadiliko ya
mazingira au athari za mazingira. Fahiwa nyingine zote za maana zinazohusiana huibuka
kutokana na maana ya msingi. Maana ya msingi pia huitwa maana ya kilekisia. kwa mfano
o kupe –mdudu anyonyaye damu
o mrija- kifaa cha kupitishia kimiminika kuelekea kwenye chombo kingine
funika- zuia kitu ili kisionekane kwa kutumia kitu kingine kama mfuniko, nguo nk
ii) Maana ya Ziada (Maana ya Kisarufi)
Ni maana ambazo huibuka kutokana na maana za msingi. Maana hizi huhusiana na
muktadha. Uelewekaji wake hutegemea muktadha ambamo neno linatumika. Kama jina
lenyewe linavyodokeza, maana ya ziada ni ziada ya maana ya kawaida/msingi. Kwa
mfano
o bosi wetu amekuwa kupe siku hizi(mnyonyaji)
o hatuwezi kupiga hatua kama taifa iwapo hatutakata mirija yote (ufisadi/ rushwa)
o katika maonesho ya Serengeti Fiesta mwaka jana, Al-Kiba alimfunika Diamond
(alimshinda)
Hata hivyo maana ya msingi na maana ya ziada zinahusiana kwa karibu sana kwani maana
ya ziada hutokana na maana ya msingi.
Aina za Maana
Wataalam wengi kama vile LEECH (1981) wanakubaliana kuwa kuna maana saba(7)
kama ifuatavyo;
i) Maana ya Msingi
ii) Maana Dokezi
iii) Maana Mtindo
iv) Maana Hisia
v) Maana Tangamani
vi) Maana Mwangwi
vii) Maana Dhamira
MAANA YA MSINGI (DENOTATIVE MEANING)
Hii ndiyo maana kuu ya neno ambayo haibadiliki kutokana na mazingira. Maana zingine zote za
ziada ambazo zinahusiana hutokana na maana hii ya msingi.aina hii ya maana huangaliwa na
kufafanuliwa kwa kigezo cha kuwapo au kutokuwapo kwa nduni bainifu (distinction features)
4
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
4
zinazokibainisha kitu hicho. Nduni hizo baininifu katika taaluma ya semantiki huitwa vijenzi
semantiki. Kwa mfano maana ya neno.
+mtu
+mtu mzima
+ke
-me
+mtu
+mtu mzima
+me
-ke
MAANA DOKEZI (CONNOTATIVE MEANING)
Hii ni maana ambayo hudokezwa na kile kisemwacho na kuwakilishwa na kinacholejelewa na
lugha. Maana hii inapatikana kwa njia ya kitu fulani kuwakilisha au kudokeza kitu fulani kingine
au hali nyingine.
Maana dokezi hutokana/huibuliwa na sifa kuu tatu:-
i) sifa za kiumbo za kitu. Hapa kinachoangaliwa ni umbo la kile kitu. Umbo hilo
huchukuliwa kukitofautisha na kitu kingine. Kwa mfano:
Mwanamke +matiti
+ujauzito
+miondoko
ii) sifa za kisaikolojia (mtu mwenyewe anavyojichukulia)- Yaani hapa
kinachoangaliwa zaidi ni ile hali ya kile kitu kisaikolojia (kwa ndani zaidi) kwa
mfano:
Mwanamke. + huruma
+ Upendo
iii) Mtazamo wa watu kuhusu kitu hicho. Yaani nini mtazamo wa watu wengi
kuhusu kitu hicho. Kwa mfano jamii inaamini kwamba:-
Mwanaume +Jasiri
+nguvu nk
Hivyo basi maana hizi zote zinategemea muktadha wa usemaji. Maneno haya
yakiwa pwekepweke huwezi kuyatolewa maana iliyokusudiwa.
MAANA YA KIMTINDO (STYLISTIC MEANING)
Maana hii huhusiana na muktadha wa matumizi ya lugha. Mitindo hiyo ni pamoja na: Mitindo
ya kilahaja, Mitindo ya kiwakati, Mitindo ya kieneo/kitaaluma/fani fulani. Mfano ‗fahamu‘ ,
Mitindo ya kiuwasilishaji, Mitindo ya kihadhi na Mitindo ya binafsi
MAANA HISIA (EFFECTIVE MEANING)
Maana hii inategemeana na inahusiana na hisia na mtazamo wa msemaji au mwandishi. Nayo
huwakilishwa kwa njia nyingi. Baadhi ya njia hizo ni:-
Mwanamke
Mwanamume
5
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
5
Kwa kutumia maana ya msingi/dokezi. Kwa mfano ‗wewe ni mwanaume kweli kweli-yaani
jasiri, shujaa nk. Au acha kulia lia kama mwanamke bwana!
Kwa kutumia njia isiyo ya moja kwa moja. Kwa mfano ‗hongera, naona leo umewahi kweli
kweli‘-huku akimaanisha amechelewa‘
Maana hisia mara nyingi hubadilika kutegemea kiimbo hata kama maneno ni yale yale. Kwa
mfano neno ‗mpole‘
MAANA TANGAMANI
Hii ni maana inayopatikana kutegemeana na muktadha wa matumizi kwa kuzingatia maeneo
mawili au zaidi yanayotangamana, yaani yanayokubali kutumiwa pamoja ili yalete maana moja.
Kwa maneno mengine maneno hayo ni maneno yanayokamilishana. Kwa mfano:-
o Mvulana-mtanashati
o Msichana-mrembo
o Usiku-kucha
o Mchana-kutwa nk
MAANA MWANGWI (MAANA AKISI) REFLECTIONAL MEANING
Ni maana inayoibuka katika hali ambapo maana moja hukonyeza maana nyingine. Yaani
humfanya mtu afikirie maana nyingine. Kwa mfano
Maana mwangwi hudhihirika katika matumizi ya tafsida mbalimbali. kwa mfano unajenga picha
gani katika sentensi zifuatazo?
o Tia basi
o Ingiza taratibu
o Hivi utanipa kweli?
o Maliza haraka basi
Kile kinachokuja akilini mwako mara baada ya kusikia ndicho huitwa maana mwangwi.
MAANA DHAMIRA
Ni maaana ambayo hutegemea kile ambacho mtoa ujumbe anakipa umuhimu. Mara nyingi
kinachopewa umuhimu hujitokeza mwanzoni mwa sentensi hivyo maana inayojengwa ni ile
inayositiriwa ndani ya sentensi. Kwa mfano
o Kikombe kimevunjwa na mtoto
o mtoto amevunja kikombe
o Kuna msichana darasani
o Darasani kuna msichana
Katika mfano wa kwanza msisitizo ni kwa kikombe lakini mfano wa pili msisitizo ni kwa
mtoto. Vivyo hivyo katika mfano wa tatu msisitizo ni msichana lakini katika mfano wa nne
msisitizo ni kujua kuwa darasani kuna msichana.
Dhana Za Msingi Katika Semantiki
i) Utajo
ii) Urejeleo
iii) Fahiwa
6
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
6
Dhana hizi tatu ni za muhimu sana katika kujifunza semantiki. Hii inatokana na ukweli kwamba
maana ya neno ‗maana‘ ni tata na uelewekaji wake hutegemea utajo wa neno, urejeleo wa neno
na fahiwa ya neno.
i) Utajo
Dhana hii inarejelea neno ‗taja‘ au ‗kutaja‘. Ni uhusiano uliopo baina ya leksimu/kyambo
(expression) na seti ya vitu ambavyo vinarejelewa na leksimu au kyambo hicho upande mmoja
una leksimu kisha upande wa pili kuna seti ya vitu vinavyolejelewa na kyambo hicho.
Kwa mfano utajo wa leksimu/kiyambo nyumba ni utajo wa vitu vyote duniani ambavyo vinaitwa
nyumba. Utajo wa kiyambo mwanafunzi wa chuo kikuu ni utajo wa kundi la watu wote ambao
kwa wakati huo wanasoma chuo kikuu. Kwa lugha nyingine utajo ni kwa ujumla.
ii) Urejeleo/reference
Urejeleo kama ulivyo utajo ni uhusiano unaohusisha viambo vya lugha na masilugha/siyo lugha.
Urejeleo unatofautiana na na utajo kwa sababu urejeleo ni uhusiano baina ya viambo vya lugha
na viwakilisho vyake duniani katika muktadha fulani maalum. Urejeleo hubainisha wazi. Kwa
mfano wanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha Dar es salaam.
iii) Fahiwa/Sense
Fahiwa ya leksimu ni seti ya mahusiano yaliyopo kati ya kiyambo hicho na viambo vingine katika
lugha. Uhusiano huo huitwa mahusiano ya kifahiwa-yaani uhusiano ndani ya lugha/maneno na
maneno ndani ya lugha. Kwa mfano unyume, usawe nk
SEMANTIKI YA KILEKSIA (lexical Semantics)
Vikoa vya maana
Msamiati wa lugha si mkusanyiko kiholela wa maneno yasiyohusiana. Wanasemantiki huamini
kuwa maneno katika ubongo wa binadamu yamepangwa katika maelfu ya makundi madogo
madogo kulingana na yanavyohusiana. Kwa mfano matunda:-kila mtu hufikiria aina mbalimbali
za matunda kwa sababu kikoa matunda kina aina mbalimbali zinazojenga kikoa hiki.
Hivyo basi, vikoa vya maana ni makundi madogo madogo ya kidhahania ya msamiati wa lugha
yaliyomo akilini mwa mwanalugha ambayo ujipangiliaji wake hutegemeana (yaani maneno hayo
yanahusiana).
Ili kudhihirisha kuwa msamiati wa lugha haupangwi kiholela, mwanafalsafa na mwanaisimu
Ferdinand de Saussure (1916) amebainisha aina mbili za maneno kimahusiano:-
1. Mahusiano ya kiwima (Paragmatic relation)
7
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
7
Ni mahusiano yanayohusu uwezekano wa neno kubadilishana nafasi na neno lingine bila
kupoteza uelewekaji wake hata kama maana itabadilika. Kwa mfano ‗mwalimu /amenunua/
kitabu/kipya/
‗Mwalimu /amenipa/ kitabu /kipya
Na huwezi kusema ‗kipya kitabu mwalimu amenipa‘ vinginevyo utaharibu mpangilio. Hivyo
chochote kinachoweza kukaa sehemu hiyo maana yake kina uhusiano.
2. Mahusiano ya Kisilisila (Kisintagmatiki) ( Sintagmatic relation)
Ni uhusiano wa maneno kimfuatano au kwa namna yanavyopangwa au kujitokeza katika tungo
kwa kuzingatia kanuni za kisarufi katika lugha husika. Kwa mfano: mtoto alikwenda shuleni
mtoto mdogo alikwenda shuleni
yule mtoto mdogo alikwenda shuleni
Vikoa vya maana Ni seti ya msamiati ambayo memba wake wanahusiana kiwima na kisilisila
(kimlalo). Kuna aina mbili za mahusiano ya maneno. Visawe vya maana vinahusiana zaidi na
mahusiano ya kiwima. Mfano wa vikoa vya maana ni kama vile
wanyama: punda, ng‘ombe, mbuzi, nk (yaani yanayohusiana)
Magonjwa: STDs: kaswende, kisonono, gonorea nk
Kikoa cha Rangi
Wataalamu wawili, Berlin na Kay walifanya utafiti katika lugha 98 na katika utafiti wao walifanya
katika rangi zinazojulikana katika lugha mbalimbali. baada ya hapo walijikita katika lugha 20
zinazoshiriki rangi mbalimbali. Katika utafiti wao waliandika kitabu kilichoitwa ‗Basic Colour
terms mwaka 1969.
Majumuisho yalikuwa kwamba:-
1) Kuna jumla ya rangi 11 ambazo zipo katika vikoa 6 na kwamba kila lugha duniani huteua
rangi zake miongoni mwa 11
2) Rangi hizi hupangiliwa kwa namna ambavyo rangi zinazotangulia upande wa kushoto
ndizo za msingi zaidi kuliko zile za upande wa kulia. Hivyo iwapo lugha itakuwa na rangi
fulani upande wa kulia basi lugha hiyo itakuwa na rangi zote zilizotangulia. Mfano wake;
1
Nyeupe
nyeusi
2
ukufu
3
Kijani
njano
4
Samawi
5
kahawia
6
Zambarau
Kijivu
Machungwa
Pinki nk,
8
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
8
3) Watoto hujifunza rangi kwa kufuata utaratibu huo. Na hapo watoto hujifunza rangi
nyeupe na nyeusi haraka. Hii inatokana na ukweli kwamba rangi hizi ziko tofauti na
zingine na wala hazikaribiani.
4) Rangi za mwisho kujifunza kwa watoto ni zile zilizomo katika kikoa cha 6. Hii inatokana
na ukweli kwamba ni vigumu sana kuzitofautisha rangi hizo na rangi zingine. Ni mpaka
watu wazima tu ndio wanaoweza kuzitofautisha zaidi.
Sifa za Vikoa vya Maana
Maneno yaliyo katika vikoa vya maana yana uhusiano wa kiusiganifu yaani yanahusiana na wakati
huo huo yanatofautiana. Kwa mfano; matunda, wanyama, samani. Hivi ni vikoa
Kikoa kimoja kikubwa huweza kujumuisha vikoa vingine vidogo vidogo
Kwa ujumla maneno katika kikoa kimoja hayana mpangilio maalum. Kwa mfano; hakuna
mpangilio maalumu katika kikoa cha matunda, yaani unaweza kuanza na tunda lolote tu.
Hata hivyo kuna vigairi, kwa mfano namba 1,2,3,4…. Siku za wiki nk. Hizi zote zina mpangilio
maalumu. Ukivuruga mpangilio huu unaharibu.
Mahusiano ya kifahiwa
Haya ni yale mahusiano yaliyopo baina ya maneno yanayounda kikoa fulani cha maana. Kuna
aina zake kama ifuatavyo:
Usinonimia (usawe), Uantonimia (unyume), Uhomonimia (neno moja maana tofauti
zisizohusiana), Upolisemia
USINONIMIA
Ni hala inayojitokeza au iliyopo pale ambapo maneno mawili au zaidi yenye maumbo tofauti na
maana moja au maana inayokaribiana. Maneno ambayo yanakaribiana au kuwa sawa huitwa
sinonimia au visawe. Kwa mfano
o Pesa, hela, fedha
o Shimo, tundu, tobo
o Mapenzi,mahaba, kupendwa
o Mjinga, bwege, mpumbavu, fala, pimbi
o Ulimwengu, dunia
Aina za sinonimia
Kuna aina mbalimbali za sinonimia, lakini hatutajadili zote bali chache tu
1. Sinonimia ya Kimantiki (Logical Synonymy)
Sinonimia hizi hutokea pale ambapo mofimu mbili au zaidi huweza kubadilishana nafasi
katika sentensi arifu zote pasipo kuathiri masharti ya ukweli. Kwa mfano
Harakaharaka-wanguwangu-upesiupesi
Kusudi-nia-lengo
Anuai-mbalimbali-tofauti tofauti
2. Sinonimia kuntu
Kwa mujibu wa Lyons (1977) anasema sinonimia kuntu hutokea pale ambapo leksimu mbili
au zaidi kuweza kubadilishana nafasi katika miktadha yote bila athari yoyote kimaana. Hata
hivyo wanaisimu wengi wanadai kwamba hadi sasa hakuna lugha yoyote duniani ambayo
9
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
9
imethibitika kuwa na sinonimia kuntu. Mtaalamu mmoja aitwaye Al Ullumani (1994) anaeleza
kuwa eneo moja ambalo linaweza kuwa na usinonimia kuntu. Ni eneo la usilabi. Kwa mfano
o Nazali na ving‘ong‘o
o Irabu na vocali
o Jitihada na juhudi
Vyanzo vya Sinonimia
Kuna mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha kutokea kwa sinonimia. Baadhi ya mambo
hayo ni:-
1. Ukopaji wa msamiati
Iwapo lugha itakopa maneno au msamiati kutoka kwenye lugha mbalimbali kuna uwezekano
kuwa na maneno tofauti au mbalimbali yanayorejelea dhana moja. Kwa mfano;
o Shule-limetoka katika Kijerumani
o Skuli-linatoka katika kiingereza
Maneno haya yanaonekana kuwa ni sinonimia lakini sababu yake ni utohoaji wa maneno kutoka
katika lugha zingine
2. jinsi / Jinsia
Maneno mengi/sinonimia nyingu hutokana na maneno yanayowarejelea wanawake au wanaume.
Kwa kawaida kuna maneno yenye maana moja ya msingi lakini matumizi yake hutofautiana kwa
sababu neno mojawapo inawarejelea wanawake na nyingine wanaume au neno moja linatumiwa
na wanawake zaidi na neno lingine likatumiwa na wanaume zaidi. Kwa mfano;
o Ujamali/utanashati-maneno haya mawili hutumika kurejelea uzuri wa sura /mwonekano
wa sura ya mwanaume. Lakini kwa upande mwingine kuna neno;
o Urembo –ambalo hutumika kurejelea uzuri wa sura au mwoneko wa mwanamke.
o Ugumba– ni neno linalotumika kurejelea hali ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa kwa
wanaume lakini kuna neno lingine la utasa ambalo linarejelea kukosekana kwa uwezo wa
kuzaa kwa mwanamke.
o Bee! (hutumiwa na wanawake katika kuitika) wakati naam! Hutumiwa na wanaume zaidi.
Lakini maana ya
msingi ya maneno haya ni kuitika.
3. Tofauti za kimaeneo/Kijiografia
Watu wanaokaa katika maeneo tofauti tofauti huweza kuwa na msamiati tofauti tofauti lakini
yanarejelea maana moja. Kwa mfano
o Ugali-hutumika zaidi Tanzania bara
o Sima-hutumika zaidi Kenya
o Sembe-ugali uliosongwa (Kongo, Lwanda, Burundi)
o Umeme-Tanzania bara
o Stimu-hutumika nchini Kenya
4. Urasmi
Hela, pesa, fedha. Kwa mfano ‗waziri wa hela‘* waziri wa fedha. Pipi na peremende
5. Ujumla na umahususi
10
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
10
Baadhi ya sinonimia hurejelea dhana za jumla na zingine dhana mahusisu. Kwa mfano:
o Hamo-nyege, kiu, Piga- zaba, charaza
6. Rika/Umri
Baadhi ya sinonimia hutumiwa zaidi kwa rika fulani. mfano watoto, wazee na watu wazima
wengine. Kwa mfano Chapa-piga (kwa mtoto unatumia chapa-mtu mzima-piga, Vibaya-dhambi
Namna ya Kutofautisha Sinonimia
i. Kuangalia miktadha mbalimbali ya matumizi ya sinonimia husika kwa kusema na
kuandika
ii. Kutunga sentensi au kava zenye sinonimia mbalimbali na kisha kubadilisha nafasi ya
sinonimia moja kwa nyingine.
UANTONIMIA/UNYUME
Unyume ni uhusiano wa kimaana baina ya maneno mawili ambapo maana ya neno moja ni
kinyume cha neno lingine au ni uhusiano baina ya maneno mawili ambapo neno moja linakigenzi
semantiki pambanuzi ambacho hakimo katika neno lingine. Maneno ambayo yana aina hiyo ya
uhusiano huitwa antonimia au vinyume. Kwa mfano: Mwanamke-mwanamume, Kubwa-ndogo,
Mbele –nyuma na Nenda-rudi
AINA ZA UNYUME
i. Unyume Kamilishani
Huu ni unyume ambao una mpaka usiopitika ambapo kukanusha upande mmoja maana yake ni
kukubali upande wa pili. Kwa mfano Mwanamke-mwanaume (maana kama wewe siyo
mwanamke ni mwanaume. Mfu-hai (maana kama wewe siyo mfu basi uko hai)Ndani-nje (maana
kama wewe hauko ndani basi uko nje)
ii. Unyume kadirifu (kadiria) Gradable antonym
Huu ni unyume ambao hauna mpaka usiopitikika na hivyo huweza kuelezwa kwa makadiriao kati
ya pande mbili husika. Kwa mfano Kubwa-ndogo (kama siyo kubwa, siyo lazima iwe ndogo)
Nene-embamba (ukisema fulani si mnene si kwamba umesema mtu huyo ni mwembamba) Zitoepesi (siyo mara zote ikiwa siyo nzito inakuwa nyepesi. Hata hivyo nafasi hizi zinakuwepo kwa
sababu ya mitazamo ya watu, kwa mfano watu wanaweza kubishana juu ya ubora wa mtu. Mtu
mwingine anaweza akasema fulani mzuri lakini pia asimaanishe kwamba ni mbaya.
Sifa ya unyume kadrifu
• Maneno katika jozi hayaligawi eneo husika katika sehemu mbili kwa uthabiti( Kunakuwa
na eneo la katikati ambalo haliwezi kurejelewa na neno lolote katika jozi, kwa mfano
mnene-mwembamba-inawezekana akawa siyo mnene na wala siyo mwembamba, hivyo
kuna maneno mengine.
• Huweza kutumia vielezi au vivumishi au vilinganishi. Kwa mfano maneno kama sana,
kabisa, mno, kuliko, kushinda, kupita, kuzidi, kama, zaidi ya, nk
• Leksimu /neno hutaja viwango tofauti vya sifa moja kulingana na muktadha husika.
Yaani ukubwa wa kitu fulani katika muktadha mmoja waweze kuwa ndiyo udogo wa kitu
kingine katika muktadha mwingine. (kwa mfano tunapozingatia wanyama tunaona
11
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
11
kwamba ndovu ni mnyama mkubwa (katika muktadha wa wanyama) hii haimaanishi
kwamba katika kila muktadha wowote ndovu atakuwa mkubwa).
• Leksimu/neno katika jozi hazina uhusiano wa usawa, yaani kukanusha leksimu moja
haimaanishi kukubali leksimu nyingine
• Katika jozi ya vinyume kadrifu ni neno moja tu ndilo liwezalo kutumika kuuliza au
kueleza kiwango au kipimo cha sifa husika. (kwa mfano ‗mbali‘ na ‗karibu‘ huwezi kuuliza
‗ukaribu kiasi gani bali utauliza ‗umbali‘. Yaani hapo ni neno moja tu linalotumika
kukadria na wala siyo maneno yote. Mfano mwingine mfupi na mrefu. Huwezi
kumwambia mtu kwamba wewe una ufupi kiasi gani bali utatumia urefu
iii. Unyume elekeani
Ni unyume unajitokeza pale ambapo uhusiano kati ya leksimu mbili katika jozi huwa ni wa
kiuelekeano. Hii ina maana kuwa leksimu moja huwa ni kinyume cha leksimu nyingine
kutegemeana na uelekeo yaani upande tendo linapoelekezwa. Kwa mfano ukisema Y ni
mume wa X maana yake ni kwamba X ni mke wa Y (Mume na mke)Ukisema Y amemkopa
X maana yake X amemkopesha Y. Mifano zaidi: Juu na chini, Panga na pangisha, ‗Nunua na
uza‘ na ‗Mbele na nyuma‘
iv. Unyume Regezi/Tenduzi
Unyume huu huhusisha jozi za leksimu ambazo maana ya leksimu moja huweza kubadilishwa
ili kurejelea kinyume chake. Kwa mfano: Ezeka-ezua, Ziba-zibua, Funga-fungua, Kunjakunjua na ‗Chomeka-chomoa‘
UHOMONIMIA
Hii ni hali ambapo umbo moja la kileksimu huwakilisha leksimu zenye maana tofauti. Hivyo
homonimia ni maneno mawili au zaidi ambayo yametokea kuwa na umbo moja au umbo
linalofanana lakini maana zake ni tofauti kabisa na hazihusiani. Kwa mfano
Kaka1—ugonjwa wa vidole
Kaka 2—-ganda la yai
Kaka 3 —-ndugu wa kiume
Panda 1—-sia mbegu
Panda 2——kwea mlima
Panda 3—-tawi
Shinda 1—-shika nafasi ya kwanza
Shinda 2—-baki mahali siku nzima
Shinda 3—-isiyojaa sawasawa
Katika kamusi homonimia huingizwa kama vidahizo tofauti
UPOLISEMIA
Ni hali ya neno moja kuwa na maana nyingi zinazohusiana.(Yule 1985). Upolisemia ni sifa ya
neno moja kuwa na maana nyingi zinazohusiana (Lyon 1977). Uhusiano uliopo baina ya maneno
12
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
12
katika upolisemia hutokana na mnyumbuliko wa maana kutoka katika maana moja ya msingi.
Kwa mfano; ‗kichwa‘-neno lina maana zifuatazo:-
a) Sehemu ya (mbele) ya mwili wa kuimbe hai yenye macho, pua,mdomo nk ambayo
hushikiliwa na shingo
b) Injini ya gari moshi inayokokota mabehewa
c) Kiongozi (mfano katika familia)
d) Mtu hodari sana (mfano katika masomo)
Neno ―Abudu‖
a) Heshimu
b) Sali
c) Nyenyekea
d) Gogopa/penda kupita kiasi
Neno ―shingo‖
a) Sehemu ya mnyama inayotenganisha kichwa na kiwiliwili ‗Miguu‘
b) Sehemu ya binadamu inayobeba kiwiliwili na hutumika kusimamia nk
UHIPONIMIA
Ni uhusiano (wa kiwima) baina ya maneno ambapo fahiwa ya neno moja hujumuisha katika
fahiwa ya neno jingine. Hii ina maana kuwa maana ya neno fulani ni sehemu ya maana kubwa au
pana ya neno lingine. neno lenye maana kubwa au pana huitwa ‗neno jumuishi‘ na lile lenye
maana ndogo au finyu huitwa ‗hiponimia‘ au( ‗maana ya neno moja imemezwa ndani ya neno
jingine) kwa mfano:-
Tukirejelea kielelezo hapo juu, neno ‗matunda‘ ndilo neno jumuishi. ndilo linalojumuiza maneno
mengine yote.
UMERONIMIA
Ni uhusiano uliopo baina ya leksimu inayotaja sehemu ya kitu na leksimu inayotaja kitu kizima
(Ni dhana inayotumiwa kueleza uhusiano wa kitu na sehemu zake na vijenzi vyake). Kwa mfano
matunda
Maembe ndizi
Dodo, mbuzi, boribo Sukari nk
13
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
13
Mwili: Kichwa, Shingo, Mabega, Tumbo, Miguu. Mfano tena ni ‘Kichwa: macho, masikio, pua,
mdomo, kinywa. Mti: mizizi, matawi nk, Gari: matairi, injini, usukani, gia, krachi, breki nk.
Tofauti ya uhiponimia na umeronimia ni kwamba uhiponimia ni uhusiano uliopo kati ya kitu na
aina zake wakati umeronimia ni uhusiano baina ya neno linaloja kitu na maneno yanayotaja
sehemu ya kitu hicho
SEMANTIKI YA SENTENSI
Hii ni Maana katika ngazi ya Sentensi. Katika semantiki ya sentensi tutajadili na kuchambua
vipengele vinavyohusu maana katika ngazi ya sentensi/tungo na mojawapo ya mambo yanayo
ukilia maana katika ngazi ya sentensi ni kanuni ya utungamanifu.
Kanuni ya ufungamanifu inasema kwamba maana ya kiambo changamani cha kisintaksia (kirai,
sentensi) inatokana na maana ya viambajengo vya kiambo hicho na mahusiano ya kisarufi.
Uhusiano wa kanuni hiyo inadhihirika pale ambapo maneno yaleyale yanatumika kuunda sentensi
zenye maana tofauti kutokana na tofauti za mahusiano ya kisarufi. Kwa mfano:-
a) Nyani alimkimbiza mtoto
b) Mtoto alimkimbiza nyani
a) Jangili amemuua nyani
b) Nyani amemuua jangili
Hata hivyo kanuni ya ufungamanifu haifanyi kazi sana katika nahau. Hii ni kwa sababu nahau ni
mafungu ya maneno ambayo maana zake mara nyingi hazitokani na muunganiko wa maana wa
maneno yanayoziunda hizo nahau. nahau si fungamanifu na mpangilio wake ni muhimu na
hauwezi kubadilishwa. kwa mfano: kuvunja ungo, kuzunguka mbuyu na kuvaa miwani. Mifano
hii ina maana ya moja kwa moja ukivuruga unatoa maana yake. Nahau zina tabia ya maneno
(yaani kuwa kama maneno na kwa sababu hii huchukuliwa kama leksimu moja na maana yake
itachunguzwa kama neno moja.)
SIFA NA MAHUSIANO YA MAANA KATIKA NGAZI YA SENTENSI/TUNGO
1. Usawe 2. Utata 3. Ukinzani 4. Upotoo 5. Uziada-dufu
USAWE
Ni uhusiano wa kimaana baina ya sentensi mbili au zaidi ambapo sentensi hizo huwa na maana
moja ya msingi. Kwa mfano ‗nilikutana na ajuza njiani‘ na ‗nilikutana na bikizee barabarani‘
Aina za Usawe
Kuna aina kadhaa za usawe kama ambavyo nitaelezea hapa chini.
Usawe wa Kileksia
14
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
14
Ni ule unaotokana na sentensi mbili au zaidi kuwa na maneno yenye maana ileile ya msingi katika
nafasi ile ile. mfano: ‗sikujua kuwa usingeongea naye Abadan au ‗sikufahamu kama
usingezungumza naye asilan.‘ Mahusiano kati ya sentensi hizo ni mahusiano ya kisinonimia.
Usawe wa Kimuudo
Hii hujitokeza pale ambapo maana ya msingi ya sentensi mbili au zaidi kubaki ile ile ingawa
sentensi hizo zina mpangilio tofauti. usawe huu ni wa kimuundo kwa sababu haugongani na
usawe wa maneno yaliyotumika. Kwa mifano: ‗Maelezo yake yalikuwa magumu kueleweka‘ na
‗ilikuwa vigumu kuelewa maelezo yake‘
UTATA
Ni hali ambapo sentensi moja huwa na maana zaidi ya moja au huweza kueleweka kwa namna
zaidi ya moja.
Aina za Utata
Utata wa Kileksika
Huu ni utata ambao husababishwa na neno au maneno fulani yaliyotumika katika sentensi
ambayo yana maana zaidi ya moja. Kwa kawaida utata wa kileksika hutokana na matumizi ya
uhonimia na upolisemia. kwa mfano: a) Baada ya shida nyingi alifanikiwa kumleta Papa nyumbani
Maana: 1. Samaki
2. papa wa kanisa katoliki
Utata wa kimuundo
Huu hutokana na jinsi sentensi zilivyopangiliwa na kutokana na umbo/neno/kirai kuwa katika
nafasi maalumu katika sentensi. kwa mfano ‗wanaume na wanawake waangalifu walikaa kando‘
maana zake:-1. Wanawake walikaa kando na pia wanaume waangalifu walikaa kando. 2.
wanawake waangalifu walikaa kando na wanaume waangalifu walikaa kando.
Mfano mwingine:- ‗Ananipenda zaidi kuliko wewe‘ Yaweza kumaanisha ‗(Yeye) ananipenda zaidi
kuliko (wewe) unavyonipenda‘ au Yeye ananipenda zaidi kuliko namna anavyokupenda wewe.
UKINZANI
Kiambo kinzani ni kile ambacho kinathihirisha vigambe (propostions) viwili siganifu wakati
mmoja. Kwa hiyo ukinzani ni hali ambayo hujitokeza pale ambapo kiambo kimoja
hunena/husema kwamba mtu au kitu fulani kina sifa fulani na wakati huo huo hakina sifa hizo.
Kwa mfano:- ‗mwanaume yule ni mwanamke kwelikweli‘ ‗mzee yule ni mtoto kabisa‘ ‗hapo hapo
nje ndipo ndani kwenyewe‘ ‗Sikujua kuandika lakini nilizawadiwa kwa kuandika makala nzuri.‘
Katika mawasiliano ya kawaida ukinzani ni suala linalopaswa kuepukwa kwani linaweza
kukwamisha mawasiliano. Hata hivyo ukinzani huweza kutumika katika muktadha maalumu kwa
sababu maalumu. Kwa mfano katika ushairi ukinzani huweza kutumika kueleza jambo lenye
ukinzani ndani yake lakini pia kulinganisha vina na mizani. Katika mazungumzo ya kawaida
unaweza kutumia kwa ajili ya kusisitiza.
15
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
15
UPOTOO/ ANOMALI
Ni ukiushi wa kimantiki unaotokea pindi vijenzi-semantiki viwili siganifu vinapounganishwa
kueleza jambo fulani. kwa mfano: ‗alichora barua kwa mguu wa kushoto (barua haichorwi-hata
kama ingekuwa inachorwa basi haitachorwa kwa mguu bali kwa mkono, hivyo kuna upotoo)
Alimpiga teke kwa kalamu nyeusi (Hatupigi tege kwa kalamu bali kwa mguu) Mjomba wangu ni
mjamzito (mjomba hawezi kubeba mimba), Rehema amemuoa Ramadhani (Mwanamke kwa
utamaduni wa Kiswahili haoi bali anaolewa) Aliandika barua kwa taa kubwa (tunaandika barua
kwa kalamu wala siyo kwa taa)
UZIADA-DUFU
Ni urudiaji usiohitajika/ usio wa lazima au ni urudiaji usiiongeza jambo jipya au taarifa mpya na
wala hauufanyi ujumbe unaotolewa kuwa wazi zaidi. Kwa mfano: ‗Mke wangu ni mke wangu!*
‗Mwanafunzi ni mwanafunzi tu* Rafiki yangu ni msichana wa kike Msikiti ule wanaswalia
waislamu ( hakuna asiyejua kwamba msikitini wanaswali waislamu)
NADHARIA ZA MAANA YA MAANA
Wataalamu mbalimbali wamebainisha nadharia mbalimbali za maana ya maana. Zifuatazo ni
baadhi ya nadharia hizo:-
1. Maana kama Kitajwa/Maana kama Kirejelewa
Nadharia hii hudai kuwa maana ya umbo la kiisimu ni kitu fulani halisi kinachotajwa na
kurejelewa na umbo hilo. Hivyo maana ya tamko ni kile kinachorejelewa na tamko hilo au kile
ambacho neno husimama badala yake. Kama umbo lolote la kiisimu lina maana basi umbo hilo
lazima liwe na kirejeleo chake. Kama maumbo mawili yanarejelea kitajwa kile kile au kitu kile kile
basi maumbo hayo yana maana moja
Ubora wake
Ni kweli yapo maneno mengi katika lugha ambayo kazi yake ni kutaja vitu mbalimbali. kwa
mfano nomino mahususi, hata baadhi ya vitenzi halisi.
Nadharia hii ina ukweli kwa kiasi fulani kwa sababu watoto wanapojifunza lugha huanza na
maumbo ya kiisimu ambayo yana vitu halisi vya kurejelea. Kwa mfano mtoto ukimtuma kikombe
anaweza akashindwa kujua lakini kama ukimwonesha anaelewa zaidi.
Dosari/udhaifu
Katika lugha kuna maneno ambayo hayana virejelewa lakini yana maana. Kwa mfano neno ‗na‘
‗hapana‘ ‗kwa sababu‘ ‗kwa‘ ‗ya‘ ‗lakini‘-maneno haya yote yana maana katika lugha ya kiswahili
lakini hatuoni kitu chochote kinachorejelewa.
Tunaweza kuwa na matamko mawili tofauti yanayorejelea kitajwa kimoja lakini si lazima
matamko hayo yawe na maana sawa kwani kuna uwezekano wa maumbo mawili sawa yakiwa na
maana tofauti. Kwa mfano:-
16
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
16
o Raisi wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
o Mwenyekiti wa CCM taifa
o Amrijeshi Mkuu wa majeshi
o Baba Ridhiwani
o Mume wa Salma
Maumbo haya yote yanarejelea ‗Jakaya Mrisho Kikwete‘
Kuna matumizi ya maneno ambayo hayarejelei kitu kinachotajwa. Kuna maneno katika lugha
ambayo hayarejelei kitu halisi. Kwa mfano neno ‗kupe‘ kama neno la Kiswahili lina kirejelewa
chake, yaani ‗mdudu‘ lakini mtu anaweza kutumia neno ‗kupe‘ akiwa na maana nyingine kabisa
kwa mfano ‗mnyonyaji‘ Baadhi ya maneno hutaja vitu dhahania na hivyo kirejeleo chake hakipo
dhahiri. Kwa mfano ‗njaa‘ ‗furaha‘ ‗huzuni‘ ‗kifo‘ ‗uhai‘ ‗zimwi‘
2. Maana kama Dhana
Nadharia hii inasema kwamba Maana ya umbo la kiisimu ni dhana au wazo linalohusishwa na
umbo hilo. Dhana ambayo imo akilini mwa mtu yeyote anayelijua umbo hilo la isimu. Kwa
mujibu wa nadharia hii maneno ni alama ya mawazo yaliyo ndani ya akili ya mzungumzaji.
Mawasiliano hufanikiwa iwapo tu maneno hayo huchochea dhana au mawazo sawa kati ya
msemaji au msikilizaji.
Watetezi wa nadharia hii wanagawa maana katika pembe tatu
Ubora
Katika nadharia hii maneno ambayo ni dhahania yanapata maana. Kwa mfano shetani, zimwi,
upendo nk
Dosari
• Baadhi ya maneno katika lugha ni vigumu kuyapatia maana na dhana yoyote. Ambayo
ama kwa hakika katika nadharia hii hayana maana kwa mfano. ‗na‘ kwa, lakini nk(maneno
haya hayana dhana)
• vile vile, mawazo au dhana ya mtu haisaidii kutambulisha maana au dhana ya kitu bali
maana ya kitu ndiyo ambayo hutambulisha mawazo ya kitu.
• Pia Maana ya neno haipatikani katika mawazo binafsi ya mtu.
• Mawazo au dhana zilizomo akilini mwa watu hazipimiki wala huwezi kuthibitisha
3. Maana kama Mwitiko/Kichocheo Mwitiko
Nadharia hii inadai kwamba tamko huwa ni kichocheo kinachoamsha mwitiko wa msikilizaji.
Hivyo maana ya tamko fulani ni ule mwitiko wa msikilizaji pindi tamko hilo linapotolewa.
Matamko mawili yatakuwa na maana sawa kama yatachochea mwitiko ule ule wa msikilizaji.
Dosari/ udhaifu/upungufu
Dhana
Alama- --- ---- ---- ---- ---- --- ---- ----urejeleo
17
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
17
• Watu huweza kuwa na miitiko tofauti kwa tamko lile lile moja katika mazingira yaleyale au
mazingira tofauti. Kwa mfano; mzungumzaji akisema ―nyoka!‖Si kwamba watu wataitika
kwa mwitiko mmoja. Kuna wengine wataitika kwa kukimbia, wengine kwa kushangaa na
wengine watashtuka huku wengine wakinyamaza na kutulia– je maana ya nyoka hapa nini?
• Kuna baadhi ya maneno katika lugha ambayo ni vigumu kuchochea mwitiko wowote kwa
msikilizaji. Maneno kama ‗na‘ ‗ya‘ ‗wa‘ nk
• Baadhi ya matamko huchochea mwitiko unaokinzana. Kuna matamko mengine yanakuja
tofauti na matarajio yake na hivyo huleta ukinzani.
• Kuna kipindi mwitiko wa mtu unaweza kuwa tofauti na vile ulivyotegemewa katika lugha.
4. Nadharia ya Maana kama Matumizi (Ludwing)
Nadharia hii iliasisiwa na Ludwing Wittgenstein katika kitabu chake cha philosophical
investigation. Alidai kuwa ni kosa kubwa mno kuweka mipaka ya maana kama ambavyo nadharia
zilizotangulia zinavyofanya. Hii ni kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuweka mipaka ya
thamani ya umbo lenyewe la kiisimu. Kwa hiyo kinachopaswa kuangaliwa ni matumizi ya umbo
hilo.
Kwa hiyo nadharia hii inasema kwamba maana ya neno ni matumizi yake katika lugha.
Wittgenstein ansema hakuna haja ya kuuliza neno hili maana yake ni nini badala yake uliza neno
hili linatumikaje? Kwa mujibu wa nadharia hii maneno kama yalivyo hayana maana isipokuwa
maana zake hujulikana wakati wa yanapotumika.
Nadharia hii inadai kuwa Maana ya neno huakisi uwezo wetu wa kulitumia neno hilo kulingana
na mfumo wa maisha yaani huakisi utamaduni wa kijamii ambamo maneno hayo yanatumika
Vile vile lugha hufungamanishwa na tabia zetu na namna zinavyohusiana na watu wengine,
tunatumia lugha kutoa amri, kuomba kitu nk. Hivyo lugha itazamwe kama chombo na wala si
kama kitu dhahania. Kwa mujibu wa nadharia hii ni kwamba maana haipo katika neno lenyewe
bali iko katika muktadha (jinsi ambavyo limetumika)
Udhaifu/changamoto
Nadharia hii ni pana mno na inatoa uhuru usokikomo kwa watumiaji wa lugha kutumia maneno
yoyote kumaanisha chochote wanachotaka kumaanisha.
Wakati mwingine nadharia hii hukwamisha maana ya maneno kwa sababu ya uhuru kupita kiasi.
Inawezekana kabisa kuzuia maana kwa sababu mtu anaweza kutumia anavyopenda.
—————————————————
Ili kujua zaidi kuhusu nadharia hizi soma Fodor (1977) na Ulliman (1962, 1964).
_______________________________
Nadharia zifuatazo nitazielezea kwa ufupi tu
5. Nadharia ya Masharti Ukweli
Hii hukitwa kwenye nadharia-tete kwamba kujua maana ya neno au sentensi ni kubainisha
masharti ambayo kwayo neno au sentensi husika itakuwa kweli au si kweli. Wasisi wa nadharia hii
ni wanamantiki na wanafalsafa baadaye ilifafanuliwa na wanaisimu. Husisitiza ukweli katika
kufasiri maana. yaani kwamba maana lazima iwe na ukweli na ukweli huo ujibainishe
wazi/bayana. Wao waligawa ukweli katika makundi kadhaa: ukweli wa Kihistoria mfano
Tanganyika ilipata Uhuru mwaka 1961, Ukweli wa Maarifa ya Ulimwengu; kwa mfano ‗Dunia
18
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
18
huzunguka jua‘ ukweli wa kiisimu. Kwa mfano Bahati aliolewa na Juma (sahihi), Juma aliolewa na
Bahati (si sahihi). Ukweli wa kiisimu hubainishwa na mantiki zilizomo katika sentensi husika.
Kwa mfano:
i. Wanaume wote hufa
ii. Seni ni Mwanaume
iii. Seni atakufa
6. Nadharia ya Ujinaishaji
Ni nadharia iliyoasisiwa na wanamapokeo ambao ni akina Plato kwa maelezo kwamba lugha
huwa na safu mbili: kiashiria na kiashiriwa. Shughuli yao kubwa ilikuwa ni kukipa kila kitu jina na
jina hilo lilitumiwa kukipa kitu hicho maana. hata hivyo nadharia hii ina udhaifu mkubwa
ukiangalia kwa undani zaidi.
7. Nadharia ya Uelekezi
Ni nadharia iliyoasisiwa na wanafalsafa waliodai kuwa njia nzuri ya kufafanua maana ya kitu ni
kwa kuonyesha kwa kidole kile kinachorejelewa. Kwa mfano
Lile ni bakuli
8. Nadharia ya Taswira
Taswira ni picha iliyomo akilini mwa mtumiaji wa lugha kuhusu kile kinachorejelewa. Nadharia
hii huchukulia kuwa kila mtu huwa na picha ya kitu anachoongelea. Wao hudai kuwa maana ya
kiashiriwa hutokana na picha au taswira inayohusiana na kiashiriwa hicho akilini mwa
mwanalugha.
PRAGMATIKI/MAANA YA ZIADA
Baadhi ya wataalamu wamedai Pragmatiki inashughulikia maana kadri inavyokusudiwa na
msemaji au anayeandika. Yaani msemaji kwa kusema hivyo anamaanisha kitu gani?
Maana na Chimbuko la Dhana ya Pragmatiki
Maana ya Pragmatiki hujadiliwa kwa kupitia vipindi mbalimbali. Japokuwa dhana hii kabla ya
miaka ya 1980 ilishughulikiwa zaidi katika taaluma ya falsafa na si kama kipengele cha kiisimu,
hivyo hata wataalamu wengi walioandika kuhusu pragmatiki walikuwa wanafalsafa zaidi kuliko
wanaisimu. Hivyo kuanzia miaka ya 1980 ndipo tawi hili lilianza kuandikwa katika vitabu vya
isimu. Mwanzoni mwa miaka ya 1980 kulikuwa na fasili mbili ambazo ni:-
i) Pragmatiki ni maana katika matumizi
ii) Pragmatiki ni maana katika muktadha
Fasili hizi zinafaa kwa kuamsha mjadala ila zina dosari zake. Baadhi ya dosari hizo ni:-
Fasili hizi kama zilivyo zinajumuisha baadhi ya vipengele vya kisemantiki ndani yake na hivyo
kutufanya tushindwe kutotautisha pragmatiki na semantiki. Kwa mfano fasili ya kwanza
19
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
19
inachukulia kuwa matumizi ni msingi wa maana katika pragmatiki lakini ya pili inachukulia
muktadha ndio msingi wa maana.
Watalaamu waliojitokeza mwishoni mwa miaka ya 1980 waliboresha maana ya pragmatiki. Kwa
hiyo tutazingeza kutoka zile za kwanza.
iii) Pragmatiki ni maana ya msemaji
iv) Pragmatiki ni tafsiri ya kile kilichosemwa yaani msikilizaji
Pamoja na kujitahidi kuboresha ufafanuzi, bado kuna udhaifu. Tatizo la fasili ya 3 ni kwamba
inamwangalia zaidi msemaji/mtoa ujumbe na kusahau kwamba upatikanaji wa maana ni
mchakato shirikishi ambao unapitia ngazi kadhaa, yaani kuanzia katika maana dhahania mpaka
katika maana ya kimuktadha. Na hivyo maana hii inamfanya mtoa ujumbe kuwa mmiliki wa
maana kitu ambacho si kweli.
Fasili ya 4 pia ina udhaifu wake kwani inazingatia mpokeaji wa ujumbe peke yake na kupuuza
vikwazo vya kijamii vinavyoweza kuwapo wakti wa mazungumzo. Kwa mfano tunaweza
kujiuliza, maana ni ya nani kati ya mpokea ujumbe na mtoa ujumbe?
Mnamo miaka ya 1980 vitabu vilivyozungumzia pragmatiki vilitoa fasili zifuatazo ambazo
tutaongeza katika fasili za nyumba:-
v) Pragmatiki ni maana ya mtagusano-fasili hii ilitolewa na Thomas (1995). Fasili hii
inaonesha kuwa maana haijikiti katika maneno peke yake wala haiukiliwi (determine) na msemaji
peke yake na wala maana haigemei utashi wa msikilizaji peke yake isipokuwa yote matatu kwa
wakati mmoja, yaani; maneno yenyewe, maana ya msemaji na maana ya msikilizaji.
vi) Kwa mtazamo wa jumla pragmatiki huchunguza uhusiano baina ya viambo vya lugha na
watumiaji wa viambo hivyo.
vii) Pragmatiki ni taaluma inayohusu mahusiano yaliyopo baina ya maana ya lugha na
watumiaji wa maumbo hayo. Fasili hii imetolewa na Yule (1996).
MUKTADHA
Muktadha huchukuliwa na watu kuwa ni mahali ilihali mtazamo huo ni finyu sana kwani katika
muktadha hatumaanishi tu mahali bali ni sehemu au mahali mazungumzo yanapofanyika. Ni
sehemu tu katika muktadha. Muktadha hujumuisha mambo yafuatayo:- Msemaji, Msikilizaji, Mtu
mwingine mmoja au zaidi ya wale wanaozungumziwa, Imani zao, Falsafa zao, Mawazo yao
kuhusu wao wenyewe na kuhusu watu wengine na Mambo yaliyokwisha semwa awali, na hali
walipo, wakati wa mazungumzo, mada ya mazungumzo pamoja na masilugha nyingine.
Kwa kifupi Muktadha unahusisha:- Nani anazungumza, Anazungumza kukiwa na nani mwingine?,
Anazungumza nini?, Anazungumza wapi?, Anazungumza kwa lugha gani?na Anazungumza akiwa na
mtazamo wake yeye mwenyewe.
Dhana ya Skima
Skima ni ramani dhahania ambazo zimo akilini mwa binadamu ambazo humsaidia kupokea na
kujifunza maarifa mapya. Skima ni ramani majumui ya maarifa au utambuzi ambayo kila mtu
anayo akilini mwake. Tunatumia skima mara zote tunapopata habari/taarifa mpya. Hivyo skima
zetu huboreshwa na hurekebishwa mara kwa mara pindi tunapopata habari/taarifa mpya.
Kila mtu ana skima kadhaa akilini mwake na kwa kawaida skima ya mtu mmoja hutofautiana na
skima ya mtu mwingine. Jambo la kusisitiza ni kwamba skima hujengwa kutokana na utambuzi,
20
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
20
kwa maana ya akili ya mtu pamoja na uzoefu alio nao kuhusu maisha na mazingira
yanayomzunguka. Skima husaidia kuelewa mambo kulingana na muktadha. Kwa mfano:
Seni aliingia akajaza mahitaji yake yote ya wiki nzima huku akaweka kapu lake kwenye toroli akalipia na
kisha akalikokota hadi kwenye maegesho ya magari, kisha aka….kwa hiyo ili uweze kuyaelewa maelezo
haya lazima uwe na skima ya maelezo hayo--supermarket.
Mfano mwingine:
Kwa kaka zangu tukio hilo lilimaanisha kupata mtu wa kusaidiana naye kuchunga mifugo, kwa baba yangu
lilimaanisha kupata mtu mwingine anayeweza kutunza familia yeye awapo safarini, lakini kwa mama yangu
lilimaanisha kuwapo kwa kipindi kifupi tu cha kusubiri kabla ya kupata mkwe wa kumsaidia shughuli za
jikoni—jando na unyago.
Huwezi kujua maana ya maelezo haya kama huna skima yake. Lakini kwa mtu ambaye ana skima
na mfano wa kwanza anaweza kujua kwa urahisi kuwa ni maeneo ya supermarket na pia mfano
wa pili unaweza kujua maana yake kwa urahisi yake kuwa ni mambo ya jando na unyago.
Njia za kupata skima
Kuna njia kadhaa zinazopendekezwa kwa ajili ya kupata skima. Hizi ni baadhi yake:-
Kupokea na kuhifadhi
Hiki ni kitendo cha kuchukua taarifa mpya na kujaribu kuihifadhi bila kuifanyia mabadiliko
yoyote. Njia hii hutumika pale ambapo taarifa mpya inayopokelewa inatangamana na skima aliyo
nayo mpokea taarifa.
Kupokea na kurekebisha
Hutokea pale ambapo upatapo taarifa mpya na kuifanyia marekebisho kidogo kwa sababu
haiendani na skima yake kuhusu jambo hilo.
Kuunda upya
Njia hii inahusisha kutengeneza skima mpya pindi upokeapo taarifa mpya ambayo inatofautiana
kabisa na skima uliyo nayo na hivyo lazima kuirekebisha ili kuondoa ukinzani uliopo akilini
mwako
Aina za skima
Kuna aina nyingi za skima lakini katika kozi hii tutajadili chache tu.
Skima ya mtu/kitu (personal skimmer)
Hizi ni skima (ramani dhahania) zinazohusu sifa za mtu fulani au kitu fulani mahususi. Hii ndiyo
humsaidia mtu kutambua kitu kipya.
Skima ya tukio (event skimmer)
Hii ni skima inayohusu mchakato au shughuli au njia ya kutenda jambo au kutatua tatizo. Ni
namna dhahania anayokuwa nayo mtu juu ya namna tukio fulani linavyoweza kufanyika. Kwa
mfano kwenye arusi huwa tunatarajia kuwepo kwa mambo vitu vingi; mfano soda, beer nk. Sasa
ikitokea hakuna linakuwa tatizo
Skima ya Dhima/Wajibu
Aina hii inahusika/inahusiana na dhima/wajibu fulani katika jamii ambao wanajamii
wanategemea kutumiza katika jamii. Inahusu matarajio ya wanajamii kuhusu dhima au wajibu wa
mtu fulani katika jamii husika
Skima na Utamaduni
Maswali ya tafakuri katika kuelezea skima na utamaduni:-
21
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
21
Je skima ya watu kuhusu mtu, tukio na dhima inategemea kutokana na tofauti za kiutamaduni? Je
inawezekana kwa watu wawili kuwa na skima inayofanana kwa jambo fulani? Wanaokubali juu ya
hili hudai kuwa watu wawili ambao wamewahi kuumwa jino skima yao inafanana pia kitendo cha
kujifungua kinaweza kufanana.
Mchango wa Wanafalsafa katika Taaluma ya Pragmatiki
Taaluma ya pragmatiki kwa kiasi kikubwa imeimarishwa na kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na
wanafalsafa zaidi kuliko wanaisimu. Jambo hili limefanya baadhi ya wataalamu wahoji iwapo
pragmatiki ni taaluma ya isimu au ya falsafa. Baadhi ya wanafalsafa waliotoa mchango katika
pragmatiki wapo katika makundi mawili:-
Wanafalsafa Mantiki na Masharti-Ukweli (Alfred Tarski)
Kundi hili lilikuwa na madai kadhaa kama ambavyo tutayaelezea hapa chini. Wao waliona kuwa
kuna aina kuu tatu za sentensi; Maelezo, Maelekezo na Maswali. Kila aina ya sentensi katika
makundi haya matatu ina dhima yake maalum au msingi kama ifuatavyo:-
• Sentensi ya maelezo-hutumika kutoa taarifa fulani au kueleza wazo
• Sentensi ya maelekezo-hutumika kumtaka mtu atende jambo kama alivyoelekezwa na
msemaji hapa na hapa kuna sentensi za maombi na amri
• Sentensi ya maswali– hutumika kuhoji mambo ili kupata ufafanuzi wa jambo fulani.
Wanafalsafa wa Lugha ya Kawaida
Kundi hili liliibuka kupinga hoja/mawazo yaliyotolewa yaliyotolewa na kundi la kwanza la
wananafalsafa kuhusu lugha na mawasiliano . Kundi hili la pili ndilo lililotoa msukumo mkubwa
zaidi katika taaluma ya pragmatiki kama tunavyoijua na kuitambua leo.
Dai lao ni kuwa badala ya kung‘ang‘ania urasmi na usanifu la lugha pamoja na ukweli na usikweli
wake kama ndio msingi wa mawasiliano tunapaswa kuchunguza namna ambavyo watu wa
kawaida hufanikisha mawasiliano baina yao kwa kutumia lugha hiyo hiyo inayodaiwa kuwa ni
vurugu ili tuone wanawezaje kuwasiliana. Katika kundi hili, wanafalsafa watatu wanatajwa kuwa
ndio vinara na mashuhuri katika taaluma ya pragmatiki.
JOHN. L. AUSTIN
Mchango wake ni kuwa aliasisi nadharia ya tendo uneneni (1962)
JOHN. R. SEARLE
Yeye aliboresha nadharia ya tendo uneni iliyoasisiwa na Austin. Maboresho hayo yalifanyika
mwaka (1969, 1975)
HERBERT P. GRICE NA KANUNI YAKE YA USHIRIKIANO
Huyu ni mwasisi wa kanuni ya ushikiano katika mawasiliano (comparative principle) mwaka
(1975). Hebu sasa tuangalie kanuni hii ya ushirikiano kwa mujibu wa Grice. Grice aliasisi kanuni
ya mazungumzo iliyoitwa ‗Logic in Conversation‘ kanuni hii inasema kuwa ‗toa mchango wako
katika mazungumzo wakati wowote au unapozungumza kwa kuzingatia lengo kubalifu na
mwelekeo wa mazungumzo unayojihusisha nayo‘
Hoja inayojengwa na Grice katika kanuni ya ushirikiano ni kwamba mawasiliano hususani yale ya
mdomo ni kitendo cha ushirikiano ambao kwa namna fulani huhitaji jitihada za pamoja kati ya
msemaji na msikilizaji.
22
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
22
Dai jingine ni aidha kanuni hii inadai kuwa katika mawasiliano kunakuwa na lengo la pamoja au
seti ya malengo yanayofahamika na kila mshiriki wa mazungumzo hayo. Kanuni hii pia inadai
kwamba katika mawasiliano/mazungumzo huwa kuna uelekeo wa mazungumzo unaokubalika na
washiriki na mwelekeo huo ndio unaowawezesha wshiriki kubaini yanayohusika na yasiyohusika
katika mazungumzo hayo yaani, yanayoweza kusemwa na yasiyoweza kusemwa katika
mazungumzo hayo.
Ili mazungumzo yafanikiwe au yafahamike msemaji anawajibu wa kumsaidia msikilizaji kuelewa
kile anachosema lakini wakati huo huo msikilizaji anapaswa kufanya jitihada ya kumwelewa
msemaji.Jitihada zinazooneshwa na msikilizaji au msemaji ndizo ambazo hufanya mawasiliano
yawe shughuli ya ushirika (kushirikiana).
Kanuni Ndogo Ndogo za Kanuni Kuu ya Ushirikiano
Kanuni ya ushirikiano ya Grice inajengwa na kufafanuliwa na kanuni ndogondogo nne kama
ifuatavyo:-
1. Kanuni ya kiasi
Kanuni hii ndogo ina vikanuni vidogovidogo ndani yake ambavyo ni:-
Toa taarifa inayohitajika tu (yaani kulingana na lengo la mawasiliano) Usitoe taarifa ya zaidi
inavyohitajika (usiseme sana wala kidogo sana kiasi cha kuzuia mawasiliano.
2. Kanuni ya ukweli (Maxims of equality)
Kanuni hii ndogo ina vikanuni vingine ndani yake ambavyo ni: Usiseme lolote unaloamini kuwa
ni uongo. Usiseme neno ambalo huwezi kulithibitisha.
3. Kanuni ya Uhusiano (Maxims of relationship)
Kanuni hii ina hoja moja tu kwamba sema yale tu yanayohusiana na mada au jambo
linalozungumziwa.
4. Kanuni ya njia/jinsi/namna/ (Maxims of manner)
Kanuni hii ina vikanuni vidogo vidogo vinne ambavyo ni:
a) Epuka maneno au miundo isiyoeleweka
b) Epuka utata
c) Sema kwa ufupi
d) Sema kwa mpangilio mzuri
Ukiukwaji wa kanuni ya Ushirikiano
Grice anasema kuwa ingawa mazungumzo yanaweza kuwa na ufanisi zaidi ikiwa wazungumzaji
watazingatia kanuni ushirikishwaji lakini ukweli ni kwamba watumiaji wa lugha hukiuka kwa
makusudi kanuni zake ndogondogo. Sababu mojawapo ya ukiukwaji wa kanuni hizo ni kwamba
binadamu wana hulka ya kumaanisha kisichosemwa au kumaanisha zaidi ya kile kinachosemwa.
Hali hii ya ukiukwaji wa ushirikiano unapojikeza wasikilizaji huibua na kung‘amua maana ya
msemaji katika muktadha husika hata kama haikusemwa bayana na msemaji huyo kupitia maneno
yake. Maana zinazoibuliwa na kung‘amuliwa kwa namna hii huitwa vimaanilizi.
Dhana Ya Vimanilizi (Implicative) Kwa Mujibu Wa Baadhi Ya Wataalam
SEARLE (1969) anaeleza kuwa Vimanilizi hutokea pale ambapo ambapo wasemaji humaanisha
zaidi ya kile kinachosemwa.
23
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
23
BROWN & YULE (1983) wanasema kuwa neno kimanilizi hutumika kuelezea kile ambacho
msemaji huweza kudokeza au kumaanisha ambacho ni tofauti na kile kisemwacho moja kwa
moja.
THOMAS (1995) anafasili kimanilizi kuwa ni maana ambayo ni tofauti na pia ni ziada kwa maana
isemwayo.
OGRAD na Wenzake wanasema kimanilizi ni maana aipatayo msikilizaji kutokana na yale
yaliyosemwa hata kama maana hiyo haikuelezwa bayana katika hayo yaliyosemwa.
Hivyo kulingana na fasili hizo hapo juu tunaweza kusema kuwa kimanilizi ni:-
Kimanilizi ni yale yasiyosemwa ambayo tunayajua kutokana na yaliyosemwa
Kimanilizi ni kile kinachomaanishwa na msemaji ingawa hakikusemwa moja kwa moja.
1. Kwa mfano mzungumzaji A na B
A: Mzee yupo?
B: Gari lake halipo (amevunja kanuni ya ushirikiano) kwa sababu alipaswa kujibu hayupo.
Hivyo kimanilizi hapa ni hayupo, maana angekuwepo gari lake lingekuwepo pia.
2. Niliposikia kwamba kuna mwanafunzi amejinyonga nilijua tu kwamba anatoka Iringa.-
kimanilizi hapa ni kwamba watu wa Iringa ni wepesi kujinyonga.
Aina ya Vimanilizi
Kuna vimanilizi vya aina mbili; kimanilizi cha kaida na kimanilizi cha mazungumzo. Sasa
tutachambua kimanilizi cha mazungumzo.
1. Vimanilizi vya Mazungumzo (conversational implicate)
Ni vile ambavyo upatikanaji na uelewekaji wake hutegemea muktadha wa mazungumzo.
Vimanilizi hivi ndivyo hasa vinavyosababishwa na ukiukwaji au uvunjaji wa kanuni ndogondogo
za kanuni kuu ya ushirikiano.
Vimanilizi vya mazungumzo huweza kutokea iwapo kanuni yoyote ndogo miongoni mwa kanuni
ndogondogo miongoni mwa kanuni nne za kanuni kuu ya ushirikiano itavunjwa au itakiukwa.
Kwa mfano;
a) Utakwenda kwenye shoo ya Diamond Jumapili Usiku?
b) Nina mtihani wa fonolojia asubuhi
Kwa hiyo: jibu ambalo atalipata akilini mwake ndilo kimanilizi (yaani ‗sitakwenda’)
a) Hilo dirisha lililo wazi linapitisha baridi kali sana
b) hasemi chochote (anafunga dirisha)
kwa hiyo: kimanilizi hapa ni ombi ‘tafadhali naomba ufunge dirisha’
a) Kwani huyo ni mwanae eeh!
b) Ni mzuri ninafurahishwa naye au Ni mbaya ninakerwa naye. ( kumbe tunaweza kuwa na
vimalizi zaidi ya kimoja kutegemeana na muktadha)
a) Ina maana bumu la kwanza limeisha?
b) Unauliza makofi polisi?
c) Unashangaa vumbi stoo
d) Kwani papa ni mkatoliki?
Kwa hiyo: kimanilizi hapa ni ‘ndiyo’
2.. Vimanilizi vya Kaida
24
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
24
Hivi ni vimanilizi ambavyo utokeaji wake hautegemei muktadha wa mazungumzo. Hii ina maana
kuwa unaweza kupata kimanilizi cha kaida kutokana na kauli fulani hata bila kujua muktadha
ambao kauli hiyo ilitolewa.
Vimanilizi kaida havitegemei kanuni ya ushirikiano na hivyo havitokani na kuvunjwa au kukiuka
kanuni ndogondogo za kanuni ya ushirikiano badala yake vimanilizi hivi hutegemea maana ya
kipragmatiki inayopatikana moja kwa moja kutokana na maneno fulani fulani yanayotumika.
Baadhi ya maneno fulani/muhimu yanayotumika vimanilizi kaidi ni haya yafuatayo:-
Na, Kwa hiyo, Hata, Kwa sababu, Bado, Lakini nk
Mfano 1: Pedael ni mchaga, kwa hiyo anajua kutafuta pesa…..(kimanilizi ni wachaga wanajua
kutafuta pesa)
Mfano 2: kijana yule ni mfupi hata siyo mbishi hata kidogo….(kimanilizi ni wafupi ni wabishi)
Mfano 3: Haka kasichana wamekatoa kijijini nini,kwa sababu kanachapa kazi kwelikweli—
(kimaninilizi ni wasichana wa kijijini wanafanya kazi kwa bidii)
Mfano 4: Nakwambia katika Harusi ya Nuru hata George alikuwepo —(kimanilizi ni George
hakutarajiwa)
Mfano 5: Dereva bado hajafika? —(kimanilizi ni alitakiwa kuwa amefika)
Sababu za kukiuka au kuvunja vikanuni vya kanuni ya ushirikiano
1. Mgongani wa vikanuni
Hali hii hutokea pale ambapo mtu hujikuta amevunja kanuni nyingine katika jitihada zake za kutii
kanuni fulani inapelekea kuvunja kanuni nyingine. Kwa mfano
a) Vipi huyo mchumba wake wa sasa ni maua sana
b) Yaelekea anampenda.
Hapa mzungumzaji B anatii kanuni ya ukweli na kujikuta anavunja kanuni ya uhusiano
2. kuonesha upole au staha
katika jamii za watu wa Ulaya msichana anapokataa ombi la kutoka na mvulana na kimapenzi
huwa anajibu kwa upole kwamba ‗ I will be washing my hair tonight‘ lakini pia jambo hili
linajitokeza katika jamii zetu. Mtu anakutafutia sababu kadhaa tu badala ya kukwambia kwamba
hataki. Kwa hiyo kuna wakati mtu anaweza kuvunja kanuni fulani kwa lengo la kuonesha staha
fulani. Mfano wa mazungumzo ya mwalimu na mwanafunzi
Mwalimu: Ndo umekuja darasani saa hizi?
Mwanafunzi: Samahani mwalimu kiatu changu kilikatika ghafla njiani nikalazimika kupitia kwa
fundi kukishona ndo maana nimechelewa.
Hivyo heshima hiyo imepelekea yeye kuzungumza hivyo na kupelekea kukiuka kanuni ya kiasi
3. Kuonesha ukali au hasira/ kukosa staha
Kwa mfano:
a) Mbwa wako anang‘ata?
b) Hang‘ati
a) (anamchezea huyo mbwa na anang’atwa) alaa! Si ulisema mbwa wako hang‘ati!
b) Hang‘ati ila huyu si mbwa wangu.
4. Kuonesha msisitizo wa jambo
Kwa mfano: A: Je umeolewa?
B: Nina watoto sita
25
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
25
Hapa B anaonesha si tu kwamba ameolewa bali ameolewa na ameshafikisha watoto sita. Nia yake
ni kusisitiza na hivyo amevunja kanuni ya uhusiano.
NADHARIA YA TENDO UNENI
Nadharia hii ilianzishwa na mwanafalsafa John L. Austin (1962) katika kitabu chake cha ‘how to do
things with words’. Huyu alidai kwamba mara kuna mambo mengi tunatenda kwa kunena, yaani kwa
maneno tu tusemayo tunatenda. Kwa ujumla nadharia hii ni majibu/pingamizi dhidi ya
madai/mtazamo wa wanafalsafa mantiki na Masharti Ukweli wanaodai kwamba kazi kuu ya lugha
ni kueleza, kufafanua au kualifu mambo mbalimbali.
Katika nadharia hii Austin anafafanuna kwamba si sentensi zote hufanya kazi ya kuarifu jambo
katika lugha na pia si sentensi zote tunazoweza kupima ukweli au usikweli wake.
Pia anasema kuwa kuna sehemu kubwa ya mawasiliano ya binadamu huhusisha maswali,
mishangao, amri, na namna mbalimbali za kuelezea hisia au matakwa ya watu. Hapa alikuwa na
maana kuwa lugha hufanya kazi nyingine kama vile kushangaa au kuuliza swali. Kwa mfano:-
• Niwie radhi
• Wewe ni mhudumu hapa?
• Chipsi mayai mishikak tafadhali
Semi zote hizi haziarifu jambo na hivyo haziwezi kusema kuwa kweli au si kweli. Anaendelea kwa
kusema kuwa hata sentensi ambazo kimuundo ni maelezo si zote zote zinatumika kueleza au
kuarifu jambo na hivyo si zote zinaweza kupimwa ukweli au usikweli wake.
• Kwa hayo machache nafunga rasmi mkutano
• Nakuonya sheria zitafuata mkondo wake
• Nakukaribisha sana katika harusi yangu
• Naweka dau kwamba Brazil itanyakua kombe la dunia mwaka huu
Sentensi hizi zote hufanya kazi zaidi ya kutoa taarifa au kuelezea jambo. Sentensi hizi ni vitendo
au sehemu ya vitendo ambavyo msemaji anavisema kwa kutenda kwa njia ya kusema. Hii ina
maana kuwa kusema kwa sentensi hizo ndio kutenda kwake.
Semo Tendeshi na Vitenzi Tendeshi
Austin anasema kuwa semo tendeshi ni zile ambazo kusemwa kwake huwa ndiko kutendwa kwa
vitendo vinavyodokezwa na vitenzi vinavyotumika.
Vitenzi Tendeshi
Vitenzi tendeshi ni vitenzi ambavyo kusemwa kwake ndio kutendwa kwake. Baadhi ya vitenzi
hivyo ni kama vile: ahidi, onya, karibisha, alike, kemea, shauri, omba radhi, nk Austin anasema
kuwa si kila semo ni semo tendeshi wala si kila kitenzi ni kitenzi tendeshi. Kwa mfano vitenzi
kama vile –pika, washa gari, heshimu, oa hivi si vitenzi tendeshi.
Madai ya Tendo Uneni
Nadharia ya tendo uneni hudai kuwa viambo vya lugha vina uwezo wa kutenda aina fulani fulani
ya matendo ya kimawasiliano kuelekeza, kuahidi, kuomba radhi nk. Unenaji wa viambo hivyo
26
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
26
ndio utendaji wa matendo yanayodokezwa na vitenzi husika kaika viambo hivyo. Kila
kinachotendwa kwa kunena tu au kutoa tu semo fulani ndicho huitwa tendo uneni.
Masharti ya Tendo Uneni
Austin anasema kuwa matendo uneni hayakamiliki kwa sababu tu vitenzi tendeshi vimetumika.
Kuna masharti ya uneni ambayo lazima yatimizwe ndipo tendo uneno husika ikamilike. Yeye
anabainisha masharti sita na kuyagawa katika makundi matatu (A, B na C)
Kundi A.
• Lazima kuwe na utaratibu kaida (ambao ni universal-unaojulikana ulimwengu mzima) juu
ya utendaji wa tendo hilo na kwamba athari ya tendo hilo ijulikane mahali pote.
• Mazingira na watu wanaohusika katika uneni wa tendo husika lazima yawe muafaka
Kundi B.
• Utaratibu wa kutenda/kutekeleza tendo husika lazima ufuatwe kwa usahihi
• Utaratibu huo lazima pia ufuatwe kikamilifu.
Kundi C.
• Aghalabu wahusika wawe na mawazo huria na dhamira ya kweli ya kufanikisha tendo
husika
• Iwapo shughuli/wajibu ambao anatakiwa kutimiza baada ya tendo uneno unafahamika
basi ni lazima wahusike watekeleze.
Hali Malidhawa katika Matendo Uneni
Austin anafafanua kuwa ili tendo uneni likamilike na kukubalika ni lazima kuwe na kile alichokiita
hali malidhawa kinachohalalisha tendo husika. Hali malidhawa ni jumla ya vitendo na sifa
ambazo tendo uneni husika huhitaji ili kukidhi/ili liwe halali au litimie. Kwa kiasi kikubwa hali
malidhawa imetokezwa katika sifa ya matendo uneni.
Hali malidhawa inahusu mambo yafuatayo:-
i) Nani anayeongea/nena/uliza/anayetenda tendo uneni.
ii) Ananena nini
iii) Anasema kwa nani/anamnenea nani?
iv) Ananena wapi
v) Ananena kwa sababu/lengo gani
Kwa mfano; wewe ni nani unayenihukumu miaka 20 jela? Wewe ni nani unayenibatiza?
Miundo ya Matendo Uneni
Ili kujua vizuri miundo ya matendo uneni ni muhimu kukumbuka uainishaji wa sentensi
uliofanywa na wanafalsafa mantiki ambapo wanafalsafa hao walizigawa katika makundi matatu;
Maelezo, Maelekezo na Swali.
Miundo ya matendo uneni hupatikana kwa kuangalia kiwima au kiukinzani kati ya sentensi na
dhima ambayo sentensi hiyo inakumbatiwa/kuibeba. Miundo hii iko kama ifuatavyo:-
1. Matendo Uneni Dhahiri
Haya ni matendo uneni ambayo huonesha kiwima kati ya aina ya sentensi na dhima ambayo
inabeba. Mfano wa maelezo: Kaka yangu ni dereva wa daladala, Watanzania tumejifunza mengi
kutokana na ushindi wa Uhuru Kenyata.
Mfano wa maelekezo: Weka dawa mahali pasipofikiwa na watoto, Marufuku kutupa takataka
katika eneo hili—kimuundo si maelezo ila ni maelekezo yenye amri na ombi.
27
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
27
Mfano wa maswali; Familia yenu ina watu wangapi? Mbali na Wamasai ni watu gani wengine
wanaojihusisha na ufugaji?
2. Matendo uneni yasiyo dhahiri
Haya ni matendo ambayo aina ya sentensi haiwiani bali inakinzana. Kwa mfano:- Unaweza
kumkopesha shilinga elfu kumi—sentensi hii kimuundo ni swali lakini dhima ni ombi. Kwa hiyo
inafanya tendo uneni lisilo dhahiri. Mfano mwingine Njaa inaniuma sana—kimuundo sentensi
hii inatoa inatoa taarifa lakini dhima ni kuomba chakula.
Kwa hiyo katika muundo huu ni kuwepo kwa muundo tofauti na dhima.
Aina za Matendo Uneni
Austin (1962) ametaja aina tatu:-
1. Kile kisemwacho
Aina hii inahusu usemi wa sentensi yoyote yenye maana inayoeleweka pia iwe na kitu
kinachorejelewa.
2. Lengo la kusema/kunena
Hii inahusu lengo la kile msemaji anachokisema au anachokiongea. Lengo la kile msemaji
anakiongea kinatengeneza tendo uneni. Kwa mfano mwanafunzi anawaambia wenzake ‗mwalimu
anakuja‘—badala ya kuwaambia waache kelele, wanafunzi wanaosikia mwitiko huu wanaweza
kuitika tofauti tofauti. Wengine kwa kunyamaza, wengine kuzomea au wengine kuendelea kupiga
kelele tu.
3. Matokeo ya kisemwacho
Inahusu athari/matokeo ya kile kisemwacho kwa msikilizaji. Matokeo ya kisemwacho kwa
msikilizaji inaweza kuwa iliyokusudiwa au haikukusudiwa. Kwa ufupi aina hii inahusu majibu ya
msikilizaji kimwili,kimaneno, kisaikolojia, kiakili nk.
Aina za Matendo Uneni Zilizoboreshwa
John Searle (1975) aliboresha aina za matendo uneni. Katika uboreshaji wake alisema kwamba
kuna aina nyingi sana za matendo uneni na labda hazina ukomo. Hii ni kwa sababu aina hizo
hutegemea lengo, muktadha na lugha husika. Hivyo akapendekeza aina za ziada za matendo
uneni. Baadhi ya aina alizopendekeza ni hizi zifuatazo:-
1. Ahadi
Haya ni matendo uneni ambayo humfunga mnenaji katika utekelezaji wa kile alichokinena kwa
siku za baadaye. Mfano wa vitenzi kwa tendo uneni hii ni; tuza, ahidi, zawadi, nk lazima
utekeleze.
2. Maelekezo/ Directives
Haya ni matendo uneni ambayo hulenga kuchochea jambo fulani lifanyike na msikilizaji kama
atakavyo msemaji. Vitenzi vinavyoweza kutumika ni pamoja na; amrisha, omba, onya, shauri,
pendekeza, sihi nk. Kwa mfano;
Tunapendekeza jaribio la Pragmatiki lifanyike Alhamisi badala ya Jumatano
Nakusihi uachane na kile kivulana chako cha chuo
3. Hisia (Expressive)
Haya ni matendo uneni ambayo hudhihirisha hisia, imani, mitazamo au mawazo ya msemaji juu
ya jambo fulani. vitenzi kama vile; shukuru, pongeza, sifu, fariji, samehe nk hudhihirisha. Kwa
mfano
28
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
28
• Nimeamua kukusamehe rafiki yangu
• Nashukuru kwa wema wako
4. Matamko
Ni matendo uneni ambayo hunenwa kwake hubadili ukweli fulani wa mambo katika dunia.
Vitenzi vinavyoweza kutumika ni kama vile; jiudhuru, achisha kazi, fungua (mkutano), funga
(mkutano), hukumu, oza(mke au mume), tangaza, kupa jina nk. Kwa mfano;
• Kuanzia leo nimekuachisha kazi
• Kuanzia sasa natangaza kwamba Wiliam na Helena ni mume na mke
• Naufungua mkutano rasmi, mjisikie huru kuchangia hoja
5. Uwakilisho
Haya ni matendo uneni ambayo hueleza kile ambacho mnenaji haamini kuwa ni kweli au si kweli.
Matendo uneni ya aina hii hujumuisha maelezo, shadidia au mahitimisho kwa mfano:-
• Lulu hakumuua Kanumba
• Wanaume si waaminifu katika mahusiano
• Wasichana wa mjini hawana mapenzi ya kweli
• Wanaume siyo waaminifu katika mahusiano
• Kada yule hatapitishwa na chama chake kugombea urais na chama chake mwaka huu
• Yule mwanao wa pili wa kiume ni shoga
DHANA YA UOLEZI
Uolezi ni uoneshaji maalum wa vitu, mahali, watu, hali nk katika muktadha husika wa
mazungumzo kwa kutumia maneno (violezi) tofauti na uoneshaji wa kawaida wa kutumia viungo
vya mwili hususan vidole. Si rahisi kwa mtu asiyejua muktadha kujua ni kitu gani
kinachojerejelewa. Kwa mfano ‘ukija yeye utamkuta pale, itabidi usubiri kwa dakika 40 kisha
tutakwenda kule kuwaona wale tuwarejeshee hiki nao wapate kile. Hapa maneno yote yaliyopigiwa mstari
ni violezi.
Aina za Uolezi
Kuna aina zifuatazo za uolezi:-
1. Uolezi nafsi
Huu ni uolezi unaotumia viwakilishi vya nafsi. Uolezi huu una violezi sita (6) vinavyogawanyika
katika makundi matatu (3)
1. Kundi la nafsi ya kwanza– hapa kuna violezi ‗mimi‘ na ‗sisi‘
2. Kundi la nafsi ya pili—hapa kuna violezi ‗wewe‘ na ‗ninyi‘
3. Kundi la nafsi ya tatu—hapa kuna violezi ‗yeye‘ na ‗wao‘
Uchanganuzi wake ni kama ifuatavyo (maana yake)
Mimi/sisi-hurejelea wazungumzaji au mzungumzaji.
2. Uolezi Wakati
Hujumuisha kutambulisha kipindi tamko fulani linatolewa. Uolezi huu hutofautisha wakati wa
kutolewa tamko na wakati tamko lilipopokelewa na msikilizaji. Kwa mfano
Andika barua yako sasa hivi
o Tutaenda kesho
29
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
29
o Seni alizaliwa tarehe ishirini na sita mwezi wa Kumi na Mbili Mwaka elfu moja mia tisa
na themanini
o Nitakuja kwako Jumapili ijayo
o Habari za asubuhi
o Pia njeo za wakati katika sentensi huweza kubainisha uolezi wakati. Kwa mfano mwalimu
wetu alikuwa anachekesha
3. Uolezi Mahali
Ni aina ya uolezi ambao huashiria mahali ambapo mawasiliano yanafanyika (Muktadha). Katika
lugha ya Kiswahili kuna viashiria kadha wa kadha vinavyoashiria mahali kwa mfano: hapa, pale,
huku, kule, huko, humu, mule nk
4. Uolezi Uelekeo
Huu ni uolezi ambao hurejelea uelekeo kwa mfano
Mbele-nyuma
Kulia-kushoto
Chini juu nk
5. Uolezi Jamii
Katika aina hii ya uolezi maana ya tungo hutegemea uhusiano wa kijamii kuweza kueleweka.
Uhusiano huo hurejelewa na maneno fulani fulani ambayo hupata maana kamili yanapotumiwa
na watu wa kaida mbalimbali katika jamii.
Huonesha uhusiano wa aina mbalimbali kwa mfano cheo, hadhi au umri wa msemaji na
msikilizaji. Kwa mfano ‗ndiyo mzee nimekuelewa!‘ nk
Mahusiano ya Ukweli
Mahusiano ya ukweli yako ya aina mbili:-
Uchopezi
Udhanilizi
A. Uchopezi
Ni uhusiano wa sentensi mbili ambapo ukweli wa sentensi ya pili hudhihirisha ukweli wa sentensi
ya kwanza. Kwa mfano;
i. Daniel amemuoa Esther
ii. Esther ameolewa na Daniel
Uchopezi ni uhusiano wa sentensi ambapo sentensi moja huchopeza sentensi nyingine. Yaani
ukweli wa sentensi moja unahakikisha ukweli wa sentensi ya pili au usikweli wa sentensi ya moja
hubeba usikweli wa sentensi ya pili.
Aina za uchopezi
1. Uchopezi wa kileksia
Ni uchopezi ambao hujitokeza pale ambapo maana ya neno au leksimu moja hujumuishwa katika
maana ya neno au leksmu nyingine katika jozi ya sentensi zinazoshughulikiwa; kwa mfano
a) Jana nilikuwa machungwa
b) Jana nilikula matunda
a) majangili yalimuua tembo
b) Tembo alikufa.
30
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
30
Mfano mwingine ni kama vile;
a) Nilikula mchicha jana
b) Nilikula mboga jana
Katika mifano hii neno matunda limechopezwa katika sentensi B. tunasema hivyo kwa sababu
machungwa ni aina ya matunda na kama sentensi A ni kweli basi sentensi B pia ni kweli.
Kwa ujumla uchopezi wa kileksia hutokea pale ambapo neno fulani katika sentensi moja katika
jozi huwa na uhusiano wa kiuhiponimia na neno jingine katika sentensi ya pili katika jozi. Kwa
hiyo katika mfano A na B hapo juu neno machungwa katika A ni hiponimia ya neno matunda
katika B (Lyons (1977).
2. Uchopezi wa kisintaksia/Kimuundo
Huu ni uchopezi unaohusisha sentensi mbili zenye miundo tofauti lakini maana yake ya msingi ni
ile ile. Mara nyingi hujitokeza katika miundo tenda na utendwa. kwa mfano; a) Mtoto amevunja
chupa ya chai b) Chupa ya chai imevunjwa na (mtoto). Ingawa sentensi hizi kimuundo ni tofauti
lakini maana ya msingi ni ile ile, kwa maana ya kwamba chupa ya chai imevunjika.
Kwa ujumla katika uchopezi wa kisintaksia sentensi moja huchopeza sentensi ya pili lakini katika
uchopezi wa kisarufi sentensi mbili huchopezana.
B. UDHANILIZO
Udhanilizo ni mtazamo wa kimaana katika Pragmatiki ambapo mzungumzaji huchukulia kwamba
msikilizaji anafahamu taarifa fulani za awali kuhusu jambo linalozungumzwa kabla hujamweleza
taarifa mpya. Kwa mfano;-
o Siku hizi mumeo kaacha kunywa pombe
o Leo umechelewa na wewe
o Mtoto amepiga chafya tena
o Ameacha kuvuta bangi?
Sifa za udhanilizo
• Haubadiliki hata pale sentensi msingi inapokanushwa. Kwa mfano Seni ameingia darasani
au Seni hakuingia darasani
• Haubadiliki hata pale sentensi msingi inapobadilishwa.
• Unaweza kubadilika kutokana na uchopekaji, udondoshaji na hata upanguaji
***Mwisho wa mihadhara***
Swali la kazi ya nyumbani ya watu watano watano;
Changamoto kuu tano za kushughulikia Semantiki na Pragmatiki
Utangulizi: Kama ambavyo imebainishwa katika swali kwamba kuchambua maarifa aliyo nayo
mwanalugha ni shughuli nzuri lalkini ina changamoto nyingi sana. walau kwa uchache
tunabainisha changamoto saba.
Mosi, hifadhi ya maana. kinachoangaliwa hapa ni mahali ambapo maana ya lugha huhifadhiwa.
Wengine wanaamini kwamba maana ya lugha huhifadhiwa na mtumiaji akilini mwake lakini
wengine huamini kwamba maana ya lugha huhifadhiwa katika kamusi. Swali la kujiuliza hapa ni
kwamba ikiwa maana ya lugha huhifadhiwa akilini mwa mtu iweje mtu aweze kukosolewa kwa
madai kwamba kamusi haisemi hivyo? Ikiwa maana inahifadhiwa katika kamusi, je waliotunga
31
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
31
kamusi walizipata wapi maana hizo? Je kamusi ina maana ya msamiati wote wa lugha? Na kama
neno halipo kwenye kamusi ina maana watumiaji wa lugha hawalitumii neno hilo kwa sababu
halina maana? maswali haya yanaonyesha ugumu mkubwa wa kushughulikana na Semantiki na
Pragmatiki.
Pili, maana ya maana. Neno maana, maana yake ni nini? Ni dhahiri kwamba neno maana
linadokeza fahiwa nyingi sana. Kuna nadharia nyingi zinazoelezea juu ya maana ya maana. kwa
hiyo hakuna maana moja. Jambo hili linaleta ugumu sana katika kushughulika na semantiki na
Pragmatiki kwani ni maana ipi ichukuliwe kuwa ndiyo maana ya maana.
Tatu, ufasili wa maana. katika hoja hii tunachokiangalia ni kwamba tunawezaje kufasili maana
ya maneno mbalimbali. Hii inatokana na kwamba kuna urudiaji wa maneno usoukomo. Ili ueleze
maana ya neno moja unahitaji kueleza maana hiyo kwa kutumia maneno mengine. Swali, je
unajuaje kwamba msikilizaji anajua maana ya maneno hayo? Na je unajuaje kwamba ufafanuzi
wako wa kutoa maana ya neno fulani ni sahihi au sisahihi?
Nne, umiliki wa maana. hapa tunachoangalia ni kwamba maana ni ya nani hasa? Je ni ya
msemaji? Na kama ikiwa maana ni ya msemaji kwa nini inafika mahali msemaji anasema ‗mimi
sikumaanisha hivyo?‘ kama maana ni ya msikilizaji, je kwa nini kuna wakati msikilizaji anasema
mimi sielewi unachosema?
Tano, kipashio cha Msingi. Hapa tunajiuliza maswali kwamba kipashio cha msingi cha
semantiki ni kipi? Kuna baadhi ya wataalamu husema kuwa ni neno (jambo ambalo haliwezekani)
na wengine husema kwamba hakuna kipashio cha msingi cha kisemantiki. Sasa tunawezaje
kuchambua maana pasipo kujua kipashio cha msingi?
Sita, mipaka kati ya Semantiki na Pragmatiki. Hapa tunachohitaji kujiuliza ni kwamba kuna
mpaka dhahiri kati ya semantiki na pragmatiki? Au mipaka iliyopo ni ya kiuchambuzi tu? Je watu
wanapozungumza hufikia wakati wanajua kwamba sasa naingia Pragmatiki?
Saba, pengo la Kileksika. Ni wazi kwamba hakuna lugha yoyote duniani ambayo inajitosheleza
kimsamiati kuweza kuelezea kila dhana. Hivyo kila lugha ina pengo la kileksika. Swali la kujiuliza
hapa sasa ni je, lugha inapokosa msamiati wa kutaja dhana fulani kuna mbinu gani inatumika
kutaja dhana hiyo? Mbinu hiyo nani aliiweka?
Hitimisho
Kutokana na hoja hizo hapo juu ni wazi kwamba si rahisi kujishughulisha na Semantiki na
Pragmatiki katika uhalisia wake bali itabaki kuwa katika nadharia tu.
Uchambuzi wa sinonimia
1. Sinonimia: inua, nyanyua, nyakua
Utofauti: Inua ni wakati sehemu tu ya kitu inakuwa juu wakati nyanyua sehemu yote ya kitu
inakuwa juu na hakuna sehemu itabaki kuwa chini lakini nyakua ni sehemu yote ya kitu itakuwa
juu lakini tendo linafanyika kwa haraka sana.
Ufanano: zote humaanisha kuweka juu kitu
2. Sinonimia: Cheo, Madaraka na Wadhifa
Utofauti: cheo ni ngazi, ajira au madaraka. Ni ngazi ya kimuundo ambayo hutegemea elimu na
ufanisi wa mtu lakini madaraka ni nguvu za kiutendaji kazi alizo nazo mtu kutokana na cheo
chake lakini wadhifa ni haki inayofungamana na madaraka aliyo nayo mtu kutokana na cheo
chake. Ni hadhi ya kijamii
32
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
32
Ufanano: zote zinahusu mtu kupata heshima fulani
3. Sinonimia: pikipiki na bodaboda
Utofauti: pikipiki ni kwa ajili ya matumizi ya jumla lakini bodaboda ni kwa ajili ya biashara
(kubeba abiria)
Ufanano: zote hutumia matairi mawili na mota ya kutumia mafuta. Zote ni pikipiki lakini
si pikipiki zote ni boda boda
4. Sinonimia: Uso na Sura
Utofauti: Uso ni halisi ni kitu kinachoshikika (complete) lakini sura ni dhahania na
haishikiki.
Ufanano: zote hurejelea sehemu ya mbele ya kichwa cha mnyama (hasa binadamu)
5. Eleza tofauti kati ya sinonimia zifuatazo Shimo, tobo na tundu
Ufafanano wake ni uwazi tu. Kwamba vyote hivi vinazungumzia uwazi. Lakini kuna
totauti zake.
• Fahiwa ya mwelekeo. Shimo lazima uelekee chini ambapo tobo na tundu si lazima
uwazi wake uelekee chini lakini kwa shimo ni lazima
• Fahiwa ya ukomo; uwazi katika shimo lazima uwe na ukomo ilhali tobo halina
ukomo. Linapitiliza mpaka upande wa pili. Na tundu linaweza kuwa na ukomo au lisiwe
na ukomo. Kwa mfano matundu kama ya chandaria. Lakini kwa tundu kwa mfano
matundu ya choo yana ukomo.
• Uasilia-katika uasilia tunajiuliza je huo uwazi ni wa asili kama sehemu ya umbile ya
hicho kitu au ni matokeo ya uharibifu? Kwa hiyo ukijiuliza swali hili ni kuwa: shimo si
maumbile asilia ya hicho kitu, linaweza kuwa limechimbwa na wadudu fulani au
wanadamu. Pia uwazi katika tobo si wa asili bali ni matokeo ya uharibifu lakini uwazi
katika tundu ni wa asilia
• Fahiwa ya ukubwa. Ingawa fahiwa hii haina mipaka dhahiri kati ya tundu na tobo
lakini kuhusu shimo uwazi wake lazima uwe mkubwa. Hata hivyo ukubwa wake hauwezi
kupimika isipokuwa kwa watumiaji wa lugha mahususi. Kwa upande wa tobo na tundu si
rahisi kutofautisha hata hivyo tunaweza kufikiri kwamba tundu ni kubwa kuliko tobo
(hakuna makubaliano katika hili)
• Je uwazi katika miili yetu ni mashimo au matobo?
Maswali ya Semina
Swali la 1
Inadaiwa kwamba nyanja za isimu, zimepangwa kingazi ambapo katika ngazi ya chini kuna
fonolojia, ikifuatiwa na mofolojia, Sintaksia katika ngazi ya mwisho juu. Kwa kutumia taaluma ya
semantiki uliyo nayo, hakiki dai hili kwa mifano ukionesha dosari inayojitokeza na kisha pendekeza
mbadala
Jibu la kiini
Huwezi kutenganisha semantiki na nyanja nyingine za lugha kwani kila Nyanja inatarajiwa
itoe maana ya kile ambacho inakielezea na kushughulika na maana ni kushughulika na
semantiki.
33
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
33
Swali la 2
Licha ya kuwepo kwa aina kadhaa za alama katika taaluma kubwa ya semiotiki ambako semantiki
imo ndani yake, ni aina moja tu ya alama inayohusika katika mawasiliano ya binadamu. Jadili kwa
mifano kuntu.
Kiini:
• Si kweli kwamba ni ishara moja tu inayohusika katika mawasiliano ya binadamu
kwa sababu kuna alama nyingi ambazo zinatumika katika mawasiliano. Kuna
ishara za nasibu ambazo ndizo zinatumiaka katika mawasialino.
• Alama mbalimbali za nasibu zinatumika katika kuashiria vitu mbalimbali kwa ajili
ya kuwasiliana.
• Rangi zinaweza kuwasilisha ujumbe fulani
• Alama ya msalaba inaonesha ‗huduma ya kwanza‘ au ‗kanisa‘
• Ishara za ufananisho: mfano wake ni; picha, ramani ya nchi, pembe tatu,kwa
mfano kama unaenda chooni ukiona picha ya ‗mwanamke‘ unajua moja kwa moja
kwamba hapo ni choo cha wanawake
• Ishara za usababisho: zinatokea baada ya kusababishwa na kitu fulani katika
milango ya fahamu. Kwa mfano; kukunja uso-kurejelea kutokufurahishwa na
jambo fulani au kukerwa na jambo.
Hitimisho:
Lugha ya ishara imekuwa ni kama nguzo ya matumizi katika mazungumzo ya kila siku.
Huweza kubadilika kulingana na kupita kwa wakati au kulingana na muktadha fulani.
maana ya ishara haiwezi kuridhishwa kutoka katika jamii moja hadi nyingine na hivyo kila
jamii huhitaji kuwa na ishara zake.
Alama—-------------------------zinaonekana
Ishara –--------------------------mara nyingi hazionekani
Teachers comment
Si ishara peke yake zinazotumika katika lugha bali kuna namna nyingine ya kutumia
1) Kwa kuangalia ufananisho wa umbo la kitu: kwa mfano kifaru kama gari
2) Kwa kuzingatia matumizi ya kitu. Kwa mfano kizibo
3) Kwa kuangalia mwigo sauti kwa mfano nyau
4) Kwa kuangalia namba. Kwa mfano 3 ya Kiarabu ni nasibu na III ya Kirumi si
nasibu kwa sababu kuna utatu kwa ndani yake
Maneno katika sentensi. Kwa ‗mtoto mdogo amekalia kiti kipya‘ maneno haya ni nasibu
lakini ndani yake kuna ufananisho fulani japokuwa ni nasibu. Mtoto….Mdogo na wala
siyo Mtoto Kidogo nk
Swali la 3
Linganisha na linganua aina za maana kama zilivyofafanuliwa na Leech (1981) pamoja na Mwihaki
(2004) huku ukitoa mifano mingi na murua.
Swali la: 4
34
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
34
Kwa kutumia mbinu mbalimbali za kutofautisha sinonimia eleza kwa ufasaha na kwa mifano thabiti
fofauti nyeti za kimaana zilizo baina ya maeno yafuatayo: chapa, charaza, tandika, zaba, nasa,
kunguta, kafua, nyuka, twanga na timba (katika muktadha wa kumwadhibu mtu kwa kumpiga)
Mbinu za kutambua na kutoafautisha sinonimia
a) Kwa kuangalia mantiki
b) Kwa kuangalia muktadha wa matumizi
• Ukubwa wa pigo
• Kifaa kinachotumika /kutangamana kwa maneno hayo. Neno zaba
linatangamana na viboko na neno charaza linatangamana na fimbo na neno
tandika linatangamana na mkwanja.
• Kushtukiza. Dhana ya kunasa ni kutaka kumshtukiza mtu. Kwa mfano unamnasa
bila yaye kuwa tayari tofauti na kumzaba kwa kumtahadharisha.
• Uzito wa kipigo-chapa ni kipigo kikubwa lakini kucharaza ni kumchapa fimbo
nyingi kama mvua.
• Lengo –lengo la kuchapa mtu ni kumtia adabu lakini lengo la kumtwanga mtu ni
kumuumiza kabisa. Mfano kama mtoto akikojoa kitandani huwezi kumtwanga.
• Lengo la kutwanga au kutimba yana fahiwa ya ule anayepigwa lazima alale chini.
Yawezekana alianza zamani kupigwa kwa hiyo kwa sababu ya kukosa nguvu basi
mtu anaamua kumtimba kwa kitu kizito kwa mfano tofauli, jiwe kubwa nk
• Kumkafua mtu unalenga kumuumiza na wala siyo kumwadhibu kwamba
abadilike.
Swali la 5
Nadharia za maana ziliibuka toka katika mtindo wa mtoano ambapo kila nadharia iliyofuata
ilijaribu kujibu mapengo yaliyoachwa na nadharia iliyotangulia. Hakiki ukweli wa dai hili kwa
kutumia nadharia za urejeleo, dhana, mwitiko na matumizi.
Kiini cha swali.
UREJELEO/kitajwa
• Maana ya umbo la kiisimu hurejelea umbo hilo.
• Maana ya tamko ni kile kinachorejelewa
• Umbo la kiisimu lazima liwe na kirejeleo chake.
• Mara nyingi inahusu majina maalum ambayo yanarejelewa.
• Kwa mfano unaweza kuwa na jina kwa upande mwingine ‗kikombe‘ na kisha kwa
upande wa pili ukawa na ‗umbo halisi la kikombe‘
MAANA KAMA DHANA
• Iliasisiwa na akina F. Dessassure, Ogrady, Sapier 1923 (aliyeasisi ni Edward Sapier
na wengine waliunga mkono hoja yake)
• Kuna uhusiano wa alama dhana na kitajwa.
• Mawasiliano hufanikiwa iwapo tu maneno hayo huchochea dhana au mawazo
sawa kati ya msemaji au msikilizaji
MAANA KAMA MWITIKO
• Iliasisiwa na Bloomfield 1935
• Maana ya tamko ni ule mwitiko
35
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
35
• Kama watu wakipokea mwitiko mmoja basi kuna maana moja
• Ubora wake ni kwamba katika lugha kuna baadhi ya maneno ambayo mwitiko
wake unafanana.
• Udhaifu wake ni kuwa inawezekana kuwa na mwitiko tofauti tofauti.
• Kuna maneno katika lugha ambayo ni vigumu kubaini mwitiko wa maneno hayo
kwa mfano maneno kama ‗na‘ ‗kwa‘ nk
• Wakati mwingine kuna mwitiko tofauti kwa jambo moja. Kwa mfano mambo –
mwingine anasema poa, mwingine ‗kwa Yesu‘
MAANA KAMA MATUMIZI
• Mwasisi wake ni Ludwing Wittgenstein katika kitabu chake cha philosophical
investigation.
• Alidai kuwa ni kosa kubwa mno kuweka mipaka ya maana kama ambavyo
nadharia zilizotangulia zinavyofanya.
• Hii ni kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuweka mipaka ya thamani ya umbo
lenyewe la kiisimu. Kwa hiyo kinachopaswa kuangaliwa ni matumizi ya umbo hilo.
• Nadharia hii ina ubora wake; lugha imefungamana na jamii.
• Lakini hata hivyo kuna baadhi ya maneno ambayo hupewa maana yake hata kabla
ya kutumiwa.
• Hakuna mipaka yoyote inayowekwa na nadharia hii
• Nadharia hii inapingana na matumizi ya kamusi ambayo inatoa maana ya maneno
bila kubainisha muktadha wa matumizi yake.
6. Vikoa vya maana ni nini? Eleza kwa mifano ya kutosha maana, sifa na umuhimu wa vikoa vya
maana katika semantiki au katika mawasiliano kwa ujumbe kisha fafanua changamoto zake katika
kuelezea maana ya maana.
Vikoa vya maana ni seti ya mahusiano. Memba hao wanaweza kuhusiana kwa namna
mbalimbali, kwa mfano unyume, usinonimia, uhiponimia, umeronimia nk ( kwa namna
nyingine haya ni mahusiano ya kifahiwa). Ni kwa namna gani usinomia unaweza
kutumika kueleza maana ya maana? Kwa mfano mtu mmoja labda hajui maana ya
wadhifa-ili kumsaidia utamwambia cheo- hapa utakuwa umetumia ujuzi wa sinonimia
katika kuelezea maana ya maana.
Au unaweza kumweleza mtu maana ya neno kwa kumweleza kinyume chake. Kwa mfano
anataka kujua nadra unamweleza kinyume chake tu.
Sifa ya vikoa vya maana
• Hakuna sifa maalumu katika kuanza. Unaweza kuanza na memba yoyote. Kwa
mfano nikitaka kusema wanyama: naweza kuanza na neno lolote kama vile sima nk
Umuhimu wa vikoa vya maana
• Husaidia kujua maana ya maneno katika lugha. Kwa mfano ili uweze kujua kikoa
cha wanyama lazima ujue baadhi ya wanyama
• Husaidia katika kujifunza lugha. Kwa mfano mtoto anapojifunza rangi huanza na
kikoa cha rangi nyeupe na nyeusi.
• Vikoa vya maana husaidia kuchanuza maana katika lugha
36
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
36
• Husaidia kuonesha umbo la wingi. Kwa mfano badala ya kusema kikoa cha tunda
tunasema kikoa cha matunda- yaani umbo la wingi ni la msingi sana katika vikoa vya
maana.
• Hurahisisha mawasiliano/huokoa muda. Kwa mfano ukifika sokoni unaweza
kusema ‗je kuna mboga za majani?‘ yaani badala ya kuuliza kwamba kuna mchicha,
maboga, mgagani, tembele nk
• Hufanikisha shughuli za wanafunzi wa leksikografia
CHANGAMOTO
• Kuna baadhi ya vikoa havina idadi maalumu kwa mfano; idadi ya siku kwa wiki,
wanyama nk
• Baadhi ya vikoa vya maana memba zake wana uhusiano wa karibu sana kiasi
kwamba ni vigumu sana kuelewa. Kwa mfano chui na dubu
• Dhana hizi ziko akilini mwa watu tu
Swali la 7:
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kungonosha maneno
mbalimbali katika mazungumzo yao. Je ungonoshaji huo ni aina gani ya mabadiliko ya maana? bainisha
kategoria zinazongonoshwa zaidi, nani hungonosha zaidi kati ya mzungumzaji na msikilizaji, sababu za
ungonoshaji huo pamoja na athari zake kijamii na kiisimu. Mifano itoke katika mikitadha tofauti tofauti.
Swali la 8
Licha ya mchango wake mkubwa katika taaluma ya maana, kanuni ya ushirikiano ya Grice (1975) ina dosari
zake. Fafanua dosari hizo kwa mifano halafu ueleze kwa mifano kuntu tofauti baina ya vimanilizi vya
mazungumzo na vimanilizi vya kaida.
Swali la 9.
Jadili dhana ya uolezi, udhanilizi, na uchopezi kama zilivyotumika katika taaluma ya Semantiki na
Pragmatiki kwa kuzingatia maana, aina na sifa zake (inapowezekana)
Swali la 10
Pragmatiki huanzia pale Semantiki inapoishia. Jadili kauli hii kwa mifano ukizingatia jinsi Semantiki na
Pragmatiki zinavyofanana, kutofautiana, kutegemeana na kukamilishana.
37
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
37
38
Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact
him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com
38
•
• Upload
•
o Masoud Issa
o
o My Clipboards
o
o My Uploads
o
o Analytics
o
o Lead Dashboard
o
o Account Settings
o
o Support
o
o Logout
•
•
• Home
• Technology
• Education
• More Topics
• My Clipboards
• For Uploaders
• Collect Leads
1 of 5
Maana ya maana!
33,736 views
• Share
• Like
• Download
Hamad Khamis Juma
, Tutor at ministry of education and vocational training
Follow
4 17 0
Published on Dec 30, 2012
3 Comments
3 Likes
Statistics
Notes
•
Clemence Ngou at Business
usawe ni maneno mengi kuwa na maana moja inyolingana au kukaribiana. kwa mfano fedha/hela/pesa.
polisemia au upolisemia ni hali ya neno moja kuwa na maana zaidi ya moja,. mfano jicho { jicho la ng'ombe, mbuzi bata} ikumbukwe kuwa upolisemia ktika kamusi haiandikwi kama kidahizo.
unyume ni hali ya kusigana kwa maneno, mfaano juu/chini. funga /fungua. njoo/nenda.
uhomonimia ni maneno yenye maana zaidi ya moja. inasimama kama kidahizo katika kamusi. mfano kaa, paa na kima.
antonimia ni sawa na unyume
1 year ago
•
Clemence Ngou at Business
MAY GOD BLESS YOU!
1 year ago
•
nelsonligaga
tafadhali nipe tofauti kati ya
hamonimia na ponisemia
usawe na unyume
antonimia na simonimia
2 years ago
Maana ya maana!
1. 1. Maana ya maana ni mojawapo ya dhana inayoibua changamoto katika nadharia za lugha(Ullman 1964:54). Kwa muda mrefu kumekuwepo na maelezo ya namna mbalimbalikutoka kwa wataalamu kama vile wanafalsa, wanasaikolojia na wanaisimu kuhusu ninimaana ya maana. Mjadala huu umekuwa na kutoelewana kwingi kati ya wataalamu hawa.Kutakana na hali hii, kubainisha maana ya maana wataalamu mbalimbali wamejaribukulipunguzia wigo na kujishughulisha na maana ya neno kwa kulipa sifa bainifu.Japo kwa kutumia kigezo hiki, ugumu wa kuelezea maana ya maana unapunguzwa kwakiasi fulani, lakini bado tatizo la msingi kuhusu nini maana ya maana lipo pale pale. Hiini kwa sababu vipashio vingi vya kiisimu (hata tukiachilia mbali maneno) vimefumbatamaana fulani. Mathalani, mofimu za maneno hufumbata maana fulani, kwani maana zamsingi zinazotokana na muunganiko wa mofimu hizo huleta maana ya jumla ya nenohusika.Katika insha hii, ‘maana’ itamaanisha mchanganyiko wa uhusiano wa kimuktadha,fonimu, sarufi, leksikografia na semantiki ambapo kila kimoja kinachangia katika maanaya msingi ya tungo kwa kuzingatia muktadha wa matumizi1.Kwa kuwa swali la “nini maana ya maana” limekuwa ni jambo la mjadala lenyekutoelewana kwingi, nadharia mbalimbali zimeasisiwa ili kujaribu kuondoa uvulivuliunaofumbatwa katika maana ya maana. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja nanadharia ya kitajwa, nadharia ya dhana, nadharia ya mwitiko na nadharia ya matumizi.Katika insha hii, nadharia ya matumizi kuhusu nini maana ya maana ndiyoitakayojadiliwa kwa mapana. Hata hivyo, nadharia nyingine zitaelezewa japo kwa ufupiili kuweka mtiririko wa mantiki.Tukianza na nadharia ya kitajwa, hii inaangalia uhusiano kati ya tungo na kitu ua vitukatika ulimwengu halisi. Kwa mantiki hii, maana ya tungo inapatikana kwa kuangaliauhusiano baina ya neno hilo na kitu kinachorejelewa. Kwa kiasi fulani, nadharia hii inaukweli ndani yake kwani kila lugha ina maneno mengi yahusuyo ulimwengu na1 Fodor (1980) 1
2. 2. malimwengu kulingana na wanajamii walivyoumega ulimwengu wao na kuainishamalimwengu yaliyomo. Hata hivyo, mtazamo huu una mapungufu fulani ikiwa ni pamojana kwamba, si kila leksimu yenye maana inarejelea kitu fulani. Yapo maneno kama vilena, sana, kwa, ni, ingawa na kadhalika yana maana pasipokuwa na virejelewa. Pili, nikwamba zaidi ya tungo moja zinaweza kurejelea kitu kile kile. Kwa mfano tungo “nyotaya asubuhi” na “nyota ya jioni” ni tungo mbili tofauti lakini zinarejelea kitajwa kimojayaani sayari ya Zuhura.Nadharia nyingine inayojaribu kuelezea maana ya maana ni nadharia ya dhana ambayoinadai kuwa, maana ya tungo ni dhana au taswira inayoibuliwa akilini mwa mtu na tungohiyo. Kwa mantiki hii, badala ya kuhusisha maana na vitu halisi moja kwa moja, nadhariahii inahusisha maana na wazo, taswira au hisia anazopata mtu pindi tungo husikaitajwapo. Upungufu wa nadharia hii ni kwamba, dhana si bainifu kwani haitabirichochote na haichunguziki. Pia, watu hupata dhana tofauti katika tungo moja.Nadharia ya mwitiko ni nadharia nyingine inayojaribu kuelezea nini maana ya maana. Hiini nadharia inayojikita kwenye mawazo ya Bloomfield (1933:139), kwamba maana yatungo ni hali ambamo msemaji hutamka tungo hiyo na mwitiko unaoibuliwa namsikilizaji. Nadharia hii inadai kuwa maana ya tungo ni lazima iwe na uhusiano namwitiko unaoendana na tungo hiyo. Hii inajaribu kuelezea uhusiano uliopo kati yawanajamii na malimwengu.Kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia hii, tungo mbili zitakuwa na maana moja kamazinatokana na uchocheo mmoja na pia kuna mwitiko sawa. Kama tukitafsiri uhusiano wauchocheo na mwitiko kwa maana ya msingi, watu wasemacho katika mazingira tofauti namwitiko wao kutoka kwa wasemacho wengine hakiwezi kuwa sawa vya kutosha kuletauhusiano huo na maana. Kasoro za nadharia hii ni pamoja na kwamba, watu huwa namwitiko tofauti katika uchocheo wa aina moja kutokana na jinsi wanavyochukuliauchocheo huo. 2
3. 3. Kwa ufupi, nadharia za kitajwa, dhana na mwitiko zinachukulia kuwa, maana ya tungo nikile kinachorejelewa na tungo au dhana inayoambatana na tungo hiyo au mwitikounaosababishwa na uchocheo wa tungo hiyo (Fodor 1980:13). Kimsingi nadharia hizihazitakuwa msingi wa insha hii.Nadharia nyingine inayojaribu kuelezea maana ya maana ni nadharia ya matumizi. Hiindiyo nadharia itakayojadiliwa kwa undani katika insha hii. Nadharia hii inahusishwamoja kwa moja na mwanafalsafa Ludwig Wittgenstein (1963:43) anayedai kuwa maanaya neno ni matumizi yake katika lugha.Kutokana na nadharia hii, ni makosa kuchukulia maana kama kitu kinachojitosheleza.Jambo la msingi ni kuangalia namna lugha inavyotumika na kwa jambo gani ua kuashirianini. Nadharia hii inazingatia kanuni ambazo zinaongoza katika kuamua matumizi aukiwango cha tungo zenye maana.Kimsingi, nadharia hii inakosoa nadharia zilizotangulia (kama zilivyoelezewa hapo juu)ambazo ni nadharia ya kitajwa, dhana na mwitiko. Katika kiwango cha semo, tunapatamaana ya tungo hiyo kutokana na jinsi ilivyotumika. Hii ina maana kwamba, maana yatungo inabainika kwa kutokana na matumizi yake.Kwa mujibu wa Wittgenstein (keshatajwa) ni makosa kujaribu kunasibisha maana katikaneno fulani au kuliwekea neno fulani maana fulani ya msingi. Kinyume chake anadaikuwa, maana ya neno au tungo inapatikana kutokana na muktadha wa matumizi, ambayoni pamoja na uelewa wa nyuma na mtazamo wa maisha ambayo wahusikawanashirikiana. Kwa mfano; tungo “amevaa miwani” inaweza kuwa na maaa ya amelewaua amevaa kitu kinachomsaidia aone vizuri au anajifanya haoni kutegemea na muktadhawa matumizi yake.Kwa mujibu wa Wittgenstein, ili kuelewa maana ya tungo fulani haina budi kuwa nauelewa mkubwa kuhusu matumizi yake ikiwa ni pamoja na imetumika wapi. Hapa 3
4. 4. anataka kuonesha jinsi muktadha wa matumizi na uhusiano wa msemaji na msemeshwajivinavyoathiri maana ya tungo. Kwa mfano, uhusiano wa kijamii kati ya wahusika.Jambo lingine la nadharia hii ni kwamba, inajihusisha zaidi na mazingira ya utumizi watungo badala kuangalia kitajwa, dhana au mwitiko vinavyorejelewa na tungo hiyo. Kwakuzingatia hoja hii, nadharia za tendo uneni na utabia zinaongozwa kwa kiasi fulani namawazo ya nadharia hii.Wittgenstein anasisitiza kuwa, lugha ina dhima nyingi na sio tu kuelezea dhana fulani aukutaja kitu fulani. Pamoja na kudokeza jambo, kuongea kunatenda vitendo ambavyo nipamoja na kuuliza, kutania, kuomba, kushawishi na kadhalika. Hapa ndipo dhana yatendo uneni, inayojaribu kuelezea jinsi watu wanavyotumia lugha na kutenda jamboinapoingia.Jambo la kuzingatia ni kwamba, kuna vitu vilivyo nje ya dhana au kitajwa. Viashiriavinavyobainisha semo kuwa ombi au amri ni pamoja na viashiria vya mwili vyamazungumzo kama vile mjongeo wa macho, midomo au mabega, kidatu, kiimbo, hadhiya kijamii na kadhalika.Kwa kuzingatia hili, tunashawishika kusema kuwa, maana ya tungo inategemeamuktadha mzima wa matumizi na sio tu katika matumzi funge. Kwa mantiki hii, dhimaya lugha katika muktadha wa kijamii inatiliwa maanani (Austin na Grice)2.Kutokana na hoja hizi, Wittgenstein anahitimisha kuwa, maana haiwezi kuelezwa kwamisingi ya utabirikaji, kwani maana inaendana na vigezo vya kijamii kuhusu ni tabia ipiya ukweli au uongo. Hoja hii inapingana na mtazamo kuwa, tunaweza kumuelezeammilisi wa lugha kama mtu anayeelewa sarufi ya lugha akilini tu.2 http:/www.shunley.eril.net/armoore/ 4
5. 5. Kwa ufupi, nadharia ya matumizi inajaribu kutatua matatizo yanayojitokeza katikanadharia zilizotangulia kwa kuzingatia muktadha wa tungo inayotumika. Hii inatokana naukweli kwamba, maana ya neno au tungo inatokana na muktadha wa matumizi yake.Kwa kuzingatia hoja hii, ni vyema kuungana na Ullmann (keshatajwa) anayeeleza kuwa,maana ichukuliwe kama mfumo wa mahusiano ya kimuktadha, fonetiki, sarufi,leksografia na semantiki.MAREJEOAustin, J. L. (1975). How to do things with words. Oxford: Oxford University PressBloomfield L (1933), Language, London-New York. Routledge and Legan PaulFloor J.D.(1980) semantics; theory of meaning in Generetive Grammar Harvad universitypress, Cambridge.Ullmann. S.(1964). Semantics: An Introdactio to the Science of Meaning. AldenPress.Oxford.http:/www.shunley.eril.net/armoore/ 5
Recommended
•
Coaching and Developing Employees
•
Solving Business Problems
•
Leadership Fundamentals
•
UTAFITI WA KIELIMU
moevt
•
Mofolojia ya kiswahili
Geophrey Sanga
•
Elimu ya Watu Wazima(EWW)
moevt
•
Uhusiano fonolojia vs mofolojia
Mwl. Mapesa Nestory
•
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Hamad Khamis Juma
•
Tamthilia ni nini?
Ignatius Ntungwa
•
Jipime Sayansi Darasa la Sita
kanguni
• English
• Espanol
• Portugues
• Français
• Deutsche
• About
• Dev & API
• Blog
• Terms
• Privacy
• Copyright
• Support
•
•
•
•
•
LinkedIn Corporation © 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni